President Lambert Tibaigana: Hatuta saidia mtu ambaye hasaidi wengine

Rais wa jumuiya ya Watanzania waishio katika jimbo la Houston, Texas Hon. Lambert Tibaigana akielezea kwa kina baadhi ya maazimio ambayo yalijadiliwa na kupitishwa na wana jumuiya hiyo na pia akigusia mambo machache ya msingi ambayo katiba ya jumuiya hiyo imezingatia.

Kama wewe ni Mtanzania unayeishi katika mji wa Houston na vitongoji vyake basi tunakuomba ujiunge na wanajumuiya wengine katika kuiendeleza jumuiya yetu. Tafadhali jiunge na jumuiya yetu, saidia viongozi wetu kwa kumtaharifu kila Mtanzania unaye mjua kuwa anaombwa ajiunge na jumuiya hii kwani inafaida sana kwa vizazi vyetu vilivyopo sasa na vijavyo! Mungu ibariki Tanzania. Mungu ibariki THC.

Leave a Reply