Reginald Mengi: I can, I must, I will

Regrann from @lemutuz_superbrand - Dk @regmengi akupa maisha yake katika kitabu

UNAWEZA kuwa na maswali mengi kuhusu Mfanyabiashara maarufu hapa nchini, Dk. Reginald Mengi,alivyoweza kufikia nafasi aliyonayo kwa sasa akimiliki makampuni kadhaa na mengine kuwa na hisa hapa nchini na ughaibuni.

Majibu ya maswali hayo na maelezo mengine yatapatikana katika kitabu chake cha kumbukumbu kuelekea utajiri ambacho kitazinduliwa Juni 30 mwaka huu.

Kitabu hicho chenye taarifa muhimu kwanza za kumfahamu Mengi ni nani kisha safari yake ndefu kufikia ustawi alionao leo akiwa na makampuni yaliyotawanyika nchini na katika nchi za majirani na mataifa tajiri duniani lakini kubwa linakupa kanuni za kufikia na kumpita pale alipofikia yeye. Usikose kitabu hiki “I Can, I Will, I Must…The Spirit of Success” (Naweza, Nitaweza, Nitafanya na Moyo wa Mafanikio)

Dk Reginald Mengi Juni 30 anazindua kitabu chenye kujaa maarifa na taarifa. Kitabu hiki kimepongezwa na wanazuoni wastaafu wa Chuo Kikuu Cha Harvard, Profess Daniel Isenberg na Profesa Sujata Bhatia kutokana na kuelezea kwa ufasaha na kiufundi mifumo ya kiuchumi na kisiasa nchini kwa miongo minne iliyopita ilivyoweza kuathiri jitihada za ujasiriamali nchini Tanzania na kuelezea nini kinahitajika katika kutafuta mafanikio.

Unaweza pia kupata updates zaidi kuelekea uzinduzi wa kitabu chake kupitia akaunti yake ya twitter @regmengi
8 days to I CAN,I MUST,I WILL book launch #iCaniMustiWill #RegMengi ‭ - #regrann

One thought on “Reginald Mengi: I can, I must, I will”

Leave a Reply