Shemeji usimchokoze baba!

Muheshimiwa shemeji, acha kumchokoza baba, au unataka vita na BabaMkwe wako ?? Baba kashasema yamekwishwa halafu wewe ndio unakuja kusoma report ??  Siunajua alisema yeye “hajaribiwi”? Wee haya wee sijui nani atasomesha wale wanao ?? …………Wapendwa msinishangae sana. Huyo anayetoa report ya sakata la Clouds Media ni shemeji yangu kabisa. Siyo wa ukoo tu, hapana! Kamuoa dada yangu kabisaaaa mtoto wa baba yangu mkubwa Samuel O. Igogo. Halafu ni shemeji ambaye nirafiki yetu sana, mkarimu usipime. Kwakweli familia yetu tumebarikiwa! Tunamshukuru Mungu……..Kwamajina anaitwa Juma Thomas ni Mwanasheria, na pia ni Journalist mkongwe. Alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa hiyo tume ya sakata la Clouds Media, ndio maana anasoma report.

Anyway, nimependa report yenu ipo fair enough! Na ushauri wenu kuhusu TCRA ni mzuri mno! Vyombo vya habari navyo vinatakiwa vilindwe kama watu wanavyo lindwa. Lazima kuwe na haki ya kulinda pande zote mbili…….Hongereni!

Leave a Reply