SIASA ZENYE MLENGO WA UCHUMI. -Peter Sarungi

SIASA ZENYE MLENGO WA UCHUMI.

Peter Sarungi (The next time)

Kuna Siasa za kuegemea uchumi (Political Economy), Siasa za kisayansi (Political Science) na Siasa za Kisanii (Political Art).

Hizi aina zote zina faida na hasara zake na kila moja ina nafasi yake katika kustawisha jamii.

Nimegundua kuwa serikali ya JPM inafanya siasa zenye kuegemea uchumi. Nasema hayo kutokana na budget ya sasa inayoonesha vipaumbele vya utawala huu ni vile vinavyo chochea uchumi ikiwa ni sector ya usafirishaji na miundo mbinu. Tunaona budget ikitupilia mbali miradi mipya ya afya, elimu, michezo, kilimo, viwanda, maji, umeme, utalii, uvuvi, ajira na kukuza sector binafsi. Budget imeweka mkazo kwenye Ujenzi, Ujenzi,Ujenzi pamoja na ununuzi wa ndege.

Kwa budget hii, fedha nyingi bado zitakwenda kwa wageni ambao watahusika na ukandarasi wa ujenzi wa Reli inayokusudiwa, ujenzi wa fly overs zinazokusudiwa na kampuni ya kutengeneza ndege. Kwa maana hiyo bado pesa haitakuwepo kwenye mzunguko wa ndani wa fedha, matokeo yake ni UKATA, UKATA. 

Aina hii ya siasa ina faida ya kukuza uchumi wa nchi na serikali yake baada ya mda wa miaka 3 na kuendelea. Serikali inakuwa na uchumi mzuri kuliko sector binafsi, Serikali inakuwa imejiingiza katika kushikilia vyanzo vya kuendesha uchumi. Ubaya wa aina hii ya siasa ni wananchi kudhoofika kiuchumi kiasi kwamba wanakuwa tegemezi kwa kila kitu kwa serikali yao. Tatizo lingine ni kwa serikali kuwa na tabia ya  kujiondoa katika kusimamia na kuendeleza miradi yenye kutoa huduma za jamii kwa wananchi wake, hili ni Tatizo kubwa sana mbeleni.

Leave a Reply