Sijawahi sema, usiamini mtu!

Wapendwa kuna mtu kani email kuniomba nimuajiri yeye kama msemaji wangu wa public  (PR)! Nikamuuliza kwanini anafikiria mimi nahitaji kuwa na msemaji wa public? Akasema mbona watu wanasema unatafuta??? Nimecheka sana!! Jamani, usiamini kila kitu unachokisikia midomoni mwa watu! Mimi kama ningekuwa nahitaji PR ningeweka tangazo hapa kwa blog! Halafu PR anifanyie kazi gani Wallah! Hii hii ya ku-blog ambayo hata Cent moja sipati au kuna nyingine?! ?? shocking! ………Yani siku hizi watu wamekuwa waongo mpaka inaogopesha! Watu ambao ukiwaona uwezi amini!! Halafu wengine ndio utakuta kila Sabato asubuhi au JumaPili wao ndio wakwanza kufungua mlango wa kanisa ?? Tuombeane jamani, siku za mwisho hizi wanasema upendo wa watu utapoa, nikweli kabisa. Watu wamekua na roho za kishetani hazielezeki! Mungu atusaidie!………..Hii blog yangu imenifanya nimejua mengi sana kuhusu Watanzania. Scary!

Leave a Reply