Siku ya walimu duniani: Leo ni siku ya walimu duniani. Je nimwalimu yupi unamkumbuka?!

Leo ilikuwa siku ya walimu duniani. Jokate akauliza je, ni Mwalimu yupi unamkumbuka?………….. Binafsi nawakumbuka walimu wangu wote kuanzia vidudu mpaka secondary lakini hawa walimu wangu wa vyuoni nawakumbu baadhi tu kwasababu ni wengi na wanakufundisha kwa semester! …….Kwa elimu yangu ya vidudu / cheke chea na grade one to two namkumbuka Mwalimu Jenifer ambaye alinifundisha vidudu pale Mgulani chini! Grade one and two namkumbuka sana Mama Mwalimu Massamu. Japo walimu wote ni muhimu sana katika kila level ya elimu lakini hawa walimu wangu wa elimu ya awali nawashukuru sana tena mno! Wanasema kuwa Mwalimu ni wito lakini kufundisha elimu ya awali ni zaidi ya wito! Mungu awabariki walimu wote duniani ambao wanafundisha kulingana na maadili ya uwalimu!

Leave a Reply