Siku zote vaa viatu kulingana na miguu yako!

Siku zote hakikisha unavaa viatu vinavyo kutosha! Usivae viatu vikubwa kuliko miguu yako ili nawe upendeke na wenye miguu mikubwa! Na usivae viatu vidogo kuliko miguu yako ili tu ufurahushe wenye miguu midogo! Na kamwe, usitembee bila viatu ili tu ukubalike na wanao penda kutembea peku peku!

Maisha ni mafupi sana lakini safari yake ni ndefu ambayo barabara yake haijulikani wapi kuna lami na wapi kuna vumbi (rough road) hivyo ni vyema kuvaa viatu vinavyo kutosha wewe mwenyewe siyo ndugu yako wala rafiki kwani wewe mwenyewe ndio utakaye tembea hiyo safari ya maisha yako. Bahati mbaya kila mtu kupangiwa bara bara yake na kila bara bara inachangamoto zake  huwezi azima viatu ambavyo hujui kama vitamudu safari yako!

Hivyo,  ili ufurahie safari yako kwanza, hepuka kuiga miondoko ya watu wengine. Wewe unaweza fikiria fulani anatembea kwa madaha ngoja niige miondoko yake  kumbe mwenzako anamaumivu ya miguu kutoka bara bara yake. Pili vaa viatu vya size yako visiwe vikubwa wala vidogo, na kama huwezi tembelea viatu virefu basi vaa viatu vya chini au boots! Mwisho, ukichoka unaruhusiwa kupumzika ila usilale bara barani hakikisha unapigania kufika mwisho wa safari.

Leave a Reply