“Sir George Kahama ni moja ya Tunu za Taifa” -Shy-Rose Bhanji

Mbunge wa bunge la Afrika Mashariki Hon. Shy-Rose Bhanji ametoa salamu zake za kuguswa na kifo cha aliyekuwa mtumishi wa umma  wa muda mrefu Sir George Kahama kwa kusema haya “Sir George Kahama ni moja ya Tunu za Taifa kwa mchango wake ktk Serikali za Mwalimu Nyerere, Mzee Mwinyi na Mkapa…Asante kwa utumishi wako uliotukuka wa kulitumikia Taifa la Tanzania. Mungu akulaze pema Baba ? Pole nyingi kwa Familia yote Mungu awape nguvu na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu #SirGeorgeKahama #RIP” ……. Muheshimiwa Shy-Rose aliyasema hayo mapema leo kupitia kurasa zake za jamii (Facebook, Instagram). Nami naomba kuungana naye kwa niaba ya familia ya mzee O.O Igogo kuwatakia pole wana familia yote, ndugu, marafiki, na jamaa. Poleni sana kwa msiba huu Mungu aendelee kuwa nanyi wakati wote……….Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe milele zote!

Leave a Reply