“Stop telling your big dreams to small-Minded people”-Steve Harvey

screenshot_2016-12-04-17-37-45-1

Ushauri umetolewa na Steve Harvey kuwa acha ku-share ndoto zako na watu wenye UFINYU wa mawazo au kwa lugha ya kisasa wanasema watu wenye MAWAZO MGANDO!………. Wanaposema “small-minded” people haina maana kuwa ni watu wenye shida ya pesa au hawana elimu! Hapana! Small-minded people niwale watu ambao hawapendi kuona mwingine anafanikiwa! Niwale watu ambao wana roho za kwanini na yuko tayari kufanya lolote lile ili kumuangusha au kumuumiza mwingine kwasababu tu ya chuki binafsi juu ya maendeleo ya mwingine! Ni watu ambao wanapenda kutoa kasoro kwa mambo ya watu bila ku-offer any solution. Ni watu ambao wanaona mapungufu ya wengine lakini si ya kwao! Ni watu ambao hufurahia anguko la mwingine. Watu wenye elimu lakini hawajaelimika! Hawezi msaidia mtu bila kunyamaza lazima watu wote wajue kuwa alikusaidia………….Kuna watu ambao ni masikini wa pesa lakini tajiri wa roho! Watu kama hawa siku zote wanaamini katika ule msemo usemao WEMA HAUOZI! Kwani kwayeye kutenda wema kwako ndipo Mungu naye atambariki katika mambo yake. Kwahiyo unaweza ukawa hauna pesa lakini una akili na roho kubwa!…,,Stop Telling Your Big Dreams To Small-Minded People!

Leave a Reply