Tuishi maisha yetu lakini tuwe na mipango endelevu ili majina yetu yasisahaulike!

Elimu juu ya maisha sio lazima ujifunze kutoka kwako au kwa wazazi wako. Muda mwingine unaweza jifunza kitu kikubwa ambacho kitabadilisha mwenendo wako au mtazamo wako wa maisha, jinsi unavyo tafakari mambo, na jinsi unavyo fanya maamuzi toka kwa marafiki au a total stranger!. Sasa Steve Harvey alijifunza kuwa njia pekee ya wajukuu na vitukuu wake kumkumbuka na kujua jina lake ni kuishi maisha yake lakini kwa wakati huo huo lazima awe na “legacy” yake ambayo hata akifa wajukuu na vitukuu wake watamjua jina lake! Na somo hili alijifunza toka kwa bibi wa rafiki yake wakati akimpa wosia kabla hajafariki.

Kuwa na mipango endelevu ni swala hata Biblia (kwa Wakristo) inatuambia ni vizuri kuwa na mipango endelevu, kuzaliana na pia kujiendeleza kiuchumi. Hii kwa Africa ilikuwa ni kuwa na watoto “wakiume” wengi kwasababu watabeba jina la baba forever, waliamini mtoto wakike akisha olewa sio wako tena na anatakiwa kuchukua jina la mumewe!! Mwe, mie shangazi zangu walisema ni mwiko kuchukua jina la mumeo kwani sio baba yako ?? shangazi zangu hakuna aliyebadilisha jina, hata dada zangu / wadogo zangu walio olewa sijaona aliyebadilisha jina. Siku hizi ni wachache sana wanafanya hivyo kutokana na carrier kuanza kubadilisha ni process ndefu sana. Hivyo wanaishia ku hyphenated. Haya nawe jifunze hilo, kama unataka wajukuu na vitukuu wako wakukumbuke anza kuwa na mipango endelevu sio kula bata tu! Kwa mfano, hawa wajukuu wa baba yangu unafikiri watamsahau babu yao? Hata kidogo! kwasababu amewapa kumbukumbu ya kudumu. Sio lazima uache mali hata mafunzo fulani ya hekima kwa wanao ambayo yataishi ndani yao milele nao wata waeleza watoto zao kuwa walifundishwa na baba / mama yake…….. Ishi maisha yako lakini uwe na mipango endelevu ili wajukuu na vitukuu vyako wakumbuke jina lako.

Leave a Reply