Ukijua umekosea basi huna budi kuomba msamaha!

Katika vitu ambavyo ni tabia yangu hata wale ambao wananifahamu vizuri na niwatu wa kuongea ukweli basi wanaweza kushuhudia hili. Mimi ni mtu ambaye nikijua nimekosea au hata kuumiza hisia za mtu mwingine basi huwa sioni haibu kuomba msamaha, kwani huo ndio ubinadamu! Kama mtu alinikwanza kiasi cha kunifanya niongee vitu ambavyo katika hali ya kawaida siwezi kuongea basi nitamwambia naomba msamaha kwa lugha niliyo tumia lakini kwamwe sito omba msamaha kwa REACTION yangu! Kwasababu REACTION yangu ipo au ilikua sahihi japo lugha yangu haikuwa sahihi! Sikumbuki kama nilisha wahi muomba mtu msamaha kwa REACTION yangu kwani mie huwa sina hulka ya kumchokoza mtu au kufanya jambo ili tu nimkwaze fulani! Pettiness is not in my vocabulary! Because I strongly believe pettiness is a ground for evil! Mtu yoyote ambaye anaweza kufanya vitu fulani vyakipumbavu kwa makusudi mimi naamini mtu huyo ana viashilia vya uchawi na anaweza hata kuua mtu!

Kitakacho nidisturb sana kwenye hii kesi ama ambacho kina nidisturb kupita vitu vyote kwenye hii kesi ni jinsi jina la mume wangu linavyo kashifiiwa“- Jacqueline Mengi

Baada ya kusikiliza haya mahojiano ya Jacqueline na Millard Ayo naomba nikubali kua nilikosea sana kutoa maoni yangu bila kusikia upande wa Jacqueline! Nilisikia upande mmoja wa hii issue na kuongea na Jacqueline kwa hisia zote na kusahau kabisa kuwa siku zote kuna sehemu tatu ya jambo lolote lisemwalo! Hivyo ninakila sababu ya kusema Jacky naomba unisamehe nimekukosea sana! I’m a woman enough to admit I was wrong thus I am sincerely apologizing for the language used and negative image that I imposed on you! Naomba ieleweke siombi msamaha kwa REACTION yangu juu ya hii issue kwani 100% I stand by Dr. Reginald Mengi’s legacy! Msamaha wangu ni kwa jinsi nilikua harsh / so hard kwa Jacqueline!

Nilichogundua hapa watu tunaweza hukumu mtu asiye na hatia kabisa kwasababu ya watu waongo ambao wengine wanaaaminika katika jamii kua ni watu wema! Mimi nachukukia sana mtu muongo na mnafiki! Yani bora niishi na mchawi au mwizi huku nikijua kabisa huyu ni mchawi na yule ni mwizi hivyo natafuta njia salama ya kuishi nao! Lakini mtu muongo na mnafiki ni mtu mbaya sana, ni wakuogopwa zaidi ya ukoma! Hawa ndio wale wanaweza kukuua halafu anakuja msibani kwako kutoa hushuhuda jinsi gani mlikua mmeshibana!

Nimeongelea uongo na unafiki kwasababu angalia hawa watu walivyo kua wakidanganya watu kua Jackie anahusika na kifo cha mzee Mengi! Ndio maana kila nikitaka kuamni hisia zangu zinakataa kabisaaa! Hivyo hizi habari za kua Jacky ameweka pingamizi mahakamani nikasema basi huyu Jacky ni mkorofi anataka kuharibu Legacy ya Dr Mengi! Kumbe mtoto wa watu anapigania kuendeleza legacy ya mumewe! Dah! I’m deeply sorry Jacky. Unafiki huu, kama huyu mdogo mtu alikua na shida na kaka yake mbona hakusema wakati akiwa hai? Ameishi na marehemu miaka tisa (9 yrs) baada ya kumuoa Jacky mbona hakusema kitu?! na kwenye harusi alikuwepo?!! Inamaana wakati ule alitumia nafasi ile kumuumiza mtalaka wa marehemu (mama Mercy Mengi) kwa faida zake binafsi na sasa anatumia kifo cha kaka yake kumuumiza Jacky na watoto wa marehemu kwa manufaa yake!

Huyu baba mdogo inaelekea hata marehemu alishamuona ni “kasheshe” hivyo machale yakamcheza akataka azikwe kwenye mji wake na sio makaburi ya familia?! Kama kweli yanayosemwa na Jacky ni ya kweli basi huyu baba mdogo ndio mvuruga familia! Na kama Regina na Abdiel watamsikiliza huyu baba mdogo wakifikiria wako salama basi wanajidanganya sana! Akimalizana na Jacky atawaingilia wao atahakikisha Regina na Abdiel wanagombana huku yeye akijifanya ndio mpatanishi! Hii dhambi mnayo itenda haita waacha salama! Naona anahasira hakuandikwa kwenye Wosia, sasa sijui anafikiria kua naye ni mtoto wa marehemu?! Halafu, Regina na Abdiel how dare are you?? Mtu anaandika mambo ya kumdhihaki baba yenu halafu mnaungana naye? Eti mkidhani mnamkomoa Jacky? Si ndio mnaionyesha umma nyie ni watu wa namna gani!

Najaribu kutafakari baba yenu aliwatendea dhambi gani ambayo mnaona anastahili kukashifiwa wakati hawezi kujitetea?! Mnataka kutuambia vile vilio vya kujiinamisha mbele ya jeneza ilikua ni maigizo?! Regina mtoto wa kike muogope Mungu wewe! Hivi kumbe hautaki Legacy ya baba yenu iendele? Au kwasababu nyie hamna watoto hivyo mnafikiri mnamkomoa Jacky? Sorry, I may sound rude but I am only trying to understand what’s this “war over”?! Mbona huo WOSIA sounds right to me! Nyie mmechukua khamsini 50% na wale watoto wamepewa 50% na Jacky wala hausiki kwenye mali ambazo marehemu alichuma na mke wa kwanza? What’s this all about? We the people of Republic of Social Media we desperately want to know!! Mzee wetu alikua mtu wa Social Media he got huge family kwenye ardhi na huku mawinguni (mitandaoni) hivyo mtueleweshe huu ugomvi wa nini! Nyie wenyewe mmesha broke “family code” kwa kwenda mahakamani sasa tunataka kusikia sauti zenu mtuambie kama Jacky anadanganya au la!!

Chakushangaza Jacky hakuingilia ndoa wala kuvunja ndoa ya mama yetu Mercy Mengi kama tulivyo aminishwa hapo mwazo! Hana nawala hataki mali yoyote ambayo ilichumwa kabla yeye hajaolewa! Sasa hizi hasira zote zanini? Kwanini mnamuonea huyu dada?! Angalia anavyo ongea kwa busara na upendo kwenye hiyo interview, anawaita “hawa wote wanangu”, “watoto wetu wakubwa” mpaka marehemu mama yenu anamuita mama?!! Jamani, if that is not LOVE then what is it!! Hivi mnajua watu wangapi wanatamani wangekua na step mama mwenye roho kama ya Jacky!! Hivi mnajua kuna step mother wangapi ambao wako busy kubomoa legacy za waume zao tena wakiwa bado hai?! Seriously, you guys had the best of best and yet naona mna ZERO appreciation! Wee Abdiel, how can you let this happen? Hivi mnaachaje baba mdogo anavuruga legacy ya baba yenu namna hii?! Nasema tena hii dhambi haita waacha salama!

Jacqueline Mengi akihojiwa na Millard Ayo!

Jacky sasa tumekupata na kukuelewa! Unakila haki na sababu ya kuongea, tena zidi kuongea ili kumbu kumbu ziwekwe! Kama unasema uongo basi wajitokeze na evidence wakanushe ulichosema! Na kwamtaji huu you deserve to sit on that throne because you have Dr Mengi’s interest in your heart! Kwanza hauja mdhulumu mtu! Nakama hawato kubali kutengua hizo kauli na maneno yao waliyo andika huko mahakamani basi kataa kupatanishwa nao kabisa! Nakuanzia sasa kitu chochote kikimkuta Jacky wao ndio watakua watuhumiwa namba moja! Halafu wataona nguvu ya familia ya mzee Mengi (The Republican of Social Media 😍😍) kama itawaacha salama! Mimi nasema Dr Mengi’s Legacy Must Live On! Dr Mengi’s Legacy For Life!

Once again, I’m so sorry! Nitakuweka kwenye maombi yangu kuanzia sasa. 😘❤❤

***Shukrani za dhati kwa Millard Ayo TV kwa interview nzuri sana***

Leave a Reply