“Ukiniuliza Mimi nitakuambia huyo asiyekua lolote wala chochote Leo ndio mzuri….”~~~Rose Shaboka

Nguo unayoinunua dukani ikiwa READY MADE wakati mwingine sio rahisi kuirekebisha iwe exactly unavyotaka. Lakini nguo unayoenda kushona kwa Fundi kuanzia mwanzo ni rahisi sana kuitengeneza ikawa exactly kile unachotaka. Msichana unayetaka na kuomba mwanaume ambaye tayari ana kila kitu (ready made) hujui unachokiomba. Sio vibaya ukipata mtu ambaye ana kila kitu tayari lakini nakuambia usimkatae wala kumdharau huyo ambaye hana kitu Leo. Ukiniuliza Mimi nitakuambia huyo asiyekua lolote wala chochote Leo ndio mzuri na ukishirikiana na Mungu vizuri unaweza kumtengeneza akawa unavyotaka na anachotakiwa kuwa kirahisi sana kuliko yule ambaye ameshatengenezwa usivyotaka. Mimi kama Fundi ukiniletea hicho kitambaa ambacho hakijashonwa ni rahisi kutengeneza unachotaka kuliko ukiniletea nguo ambayo ilishashonwa kitu kingine niitengeneze iwe kitu kingine. Huyo mwanaume asiye na chochote Leo ni kitambaa kipeleke kwa Fundi anaitwa Yesu akutolee style moja matata itakayokutosha katika hali zote ambayo macho hayajawahi kuona, masikio hayajawahi kusikia wala akili za mwanadamu hazijawahi kufikiria Yale mambo Bwana amewaandalia wampendao.

#mchungaji anapokua Fundi cherehani hata kwenye vitambaa vya kushona anapata mafunuo#
#kila jambo lina majira, hata kukosa kuna mwisho hatakua maskini milele, usimdharau#
#pastors new day church, power house#
#victoria petrol station#

Leave a Reply