UKIPINGWA NA MKUU, VIZURI UKAJIWAJIBISHA. -Peter Sarungi

UKIPINGWA NA MKUU, VIZURI UKAJIWAJIBISHA!

Peter Sarungi (The next Speaker)

Ingawa ni vigumu kupata tamaduni za kuwajibika kwa viongozi wengi wa Afrika lakini bado kuna kila ulazima wa kuwakumbusha viongozi wetu na hata kuwafunza vijana ambao ni kizazi kinachochukua dhamana kutoka kwa wazee wetu juu ya umuhimu na faida za kuwajibika mwenyewe bila kushurutishwa.

Watanzania tunafunzwa na viongozi wetu kuwa na tabia za ajabu sana unapopata madaraka, tabia kama za ubabe, majivuno, dharau, ung’ang’anizi, ufisadi, uzembe na zingine nyingi ambazo tumekuwa tukizishuhudia kutoka kwa viongozi wetu. Tamko alilotoa Waziri wa Sheria la kupiga STOP ufungaji wa ndoa bila cheti cha kuzaliwa kuanzia mwezi wa tano na baada ya muda mfupi Mkuu wa kaya akatoa katazo la utekelezaji wa agilo la waziri wake. 

Kwa tafakuri ndogo, inaonesha kwamba agizo hilo la waziri halikupata utafiti wa kutosha na pia halukupita kwenye vyombo vya ushauri kama Baraza la mawaziri. Pia inaonekana agizo hilo limemkera sana Mkuu wa kaya kiasi kwamba akalitolea tamko yeye mwenyewe bila kutumia wasaidizi wake kama vile waziri aliye husika kutoa agizo hilo.

Kwa maamuzi aliyoyafanya Mkuu wa nchi kwa Waziri husika lina fundisho kubwa sana na angalizo kwa waziri husika. Ningekuwa mimi ni waziri husika ninge jiwajibisha kwa kushindwa kufikia viwango vya mkuu wangu wa kazi, maana inawezekana akanitumbua ama akanisahau kwenye marekebisho ya baraza la mawaziri.

Nafikiri ni muda mzuri kwa Waziri Mwakiyembe kuji pumzisha ikiwa ni hatua ya kujiwajibisha ili aendelee kubaki na heshima yake iliyo tukuka kwa nchi. Kuna faida kubwa ya kujiwajibisha mwenyewe kuliko kusubiri kuwajibishwa tena kwa aibu, nasema hayo kwa sababu na mimi mpaka leo naendelea kunufaika na hii tabia ya kujiwajibisha ambayo nimewahi kuifanya sehemu mbalimbali za uongozi wangu.

By the way kuna kazi sana kutoa tonge kutoka kwenye midomo ya waafrika, wapo tayari kunyang’anywa kwa nguvu kuliko kulitema wenyewe hata kama tonge ni chungu.

Asanteni.

Leave a Reply