Umesikia kuhusu Samaki bandia (wa plastic)?!

Umesikia au kuona hii?! Naamini wengi mmesikia nankuona mchele bandia sina huwakika kama wengi wameona kituko hiki! Juzi nilitumiwa video inayo onyesha mtu amenunua Samaki bandia katika moja ya maduka / supermarket ya Waafrica huko London. Kwakweli inaogopesha sanaaaaaa! Shetani ameamua kutuangamiza kwa njia ya vyakula baada ya kuona watu wanahimizwa kula vyakula bora haswa kuachana na nyama nyekundu! Embu tazama hii video ?
Kama wewe ni mmoja wa watu ambao hawachunguzi nini wanakula basi anza sasa kwani itakusaidia sana! Kama unaweza kushika na kukagua fanya tu kama huyo kaka kwenye video Nakumbuka mwanzoni mwa mwaka huu nilipokuwa nyumbani nilimfundisha sana mama yangu kuacha tabia ya kununua kitu kwa kupewa recommendation na rafiki au mwanafamilia. Kunasiku tulikuwa Supermarket, sasa kwakuwa anajua mimi huwa situmii white-bread (ile ya ngano iliyo kobolewa), sasa akabiambia hizi biscuits ni nzuri sana ni "whole wheat" tena Sugar-free  nilishawahi kuzitumia ngoja nikununulie. Sasa kabla hajanunua nikachukua package moja nakusoma maelezo yake ?? Nilipigwa na butwaa! Nikamuuliza, mama nani alikwambia hizi biscuits ni Sugar free?! Akasema dada yangu mkubwa (ninaye mfuata) ndio alimwambia. Halafu akakoleza; "tena anazipenda kweli"! ??  Nikamwambia mama mara ngapi nakwambia usome ingredients ya kitu kabla ya kununua? ?? Hizi biscuits wameandika Sugar free lakini inaaina nyingine ya Sukari ndani yake ambayo ni mbaya zaidi! Yani bora kula Sukari yakawaida ni salama zaidi ya hiyo! Mama yangu yeye miaka mingi sana hatumii Sukari, lakini hakuna kitu kibaya kama High Fructose Corn Syrup! Hii ni aina ya Sukari ambayo wengi wasiojua wanatumia lakini ni hatari sana. Ni sukari inayotengenezwa kwa mahindi na mihunzi yake. Inatumiwa sana kwenye artificial juices, and food! Baadhi ya watu wenye Diabetes wanatumia kama "surpliment" lakini ni hatari bora kuacha kutumia Sukari kabisa. Au tumia coconut syrup, honey, au maple syrup. Lakini hii Fructose Corn Syrup kaa nayo mbali!

Leave a Reply