“Usimuingize mtu shimoni kwa shida na STRESS zako” ~~~~ Zamaradi Mketema.


Wengi wanatamani harusi ila wanasahau kuna maisha ya NDOA baada ya harusi, hivyo Kabla ya kukubali maombi ya mtu hakikisha umeridhika na yote juu yake mazuri na mabaya maana ndio unayoenda kupambana nayo MILELE. Usifurahie kusema I DO bila kujua unakubali kitu gani, unapokubali pale humkubali yeye tu ila yeye na matatizo, vimbwangwa, kasoro na kila alichonacho. 

Lakini inavyoonekana Karibu wengi wako tayari kuvaa shela huku mengine wakijipa moyo kujuana nayo mbele kwa mbele, wanachosahau ndoa sio kitu cha mchezo wala majaribio, ndoa inahitaji UTAYARI na sio kukurupuka. Usiolewe kwakuwa rafiki yako ameolewa huenda yeye amepata mtu sahihi hivyo isikufanye udandie yeyote alie mbele kumbuka kila mtu ataishi nyumba yake Usiolewe kwakuwa umri wako umekata kona, badala ya kupata pumziko unaweza jikuta unamalizia uzee wako vibaya na uchungu mwingi kwa kuparamia tu ukajuta maisha yote Usiolewe kwakuwa umezaa na mtu, kama si mtu sahihi UBABA hauwezi kumbadilisha kwa namna yeyote. 

Usiolewe kwa msukumo wa wazazi, utakapoingia kwenye ndoa kama ni furaha itakuwa ya kwako na kama huzuni utasema nayo mwenyewe wao kazi yao itakuwa maneno tu ambayo hayatakuwa yanasaidia chochote kwa wakati huo. Na wala usiolewe kwakuwa EX kaoa, yeye amepata alieridhika nae na sio dhambi, sasa wewe okota tu yyeyote KUKOMOA, humkomoi mtu na utaisoma mbele kwa mbele OLEWA kwakuwa uko TAYARI na umeridhika kwa HALI YOYOTE ALIYONAYO. Kwenye harusi utakuwa special kupitiliza lkn baada ya pale usitegemee uspecial uendelee, na zaidi hakuna wa kupoteza muda kila siku na nyinyi kwenye ndoa kama walivyokuwa wanapoteza? kwenye vikao vya harusi hivyo lazima ujue jinsi ya kusimama na ya kwako. Kwenye harusi kuna michango kwenye ndoa hakuna wa kukuchangia, JIPANGE. 

lakini KUBWA hakikisha unaeingia nae kwenye ndoa UNAMPENDA KWA DHATI maana ndie utalala na kuamka nae kwa muda wote wa maisha yako, sasa kama utaamua kujibana kwa usiempenda kwa ajili ya visababu fulani jua hujiumizi wewe pekee ila utaitesa hata nafsi ya anaekupenda isiyo na hatia kwa kumfanyia YASIYOSTAHILI maana hutaweza kuigiza milele, kumbuka Hakukuoa ili ATESEKE, usimuingize mtu shimoni kwa shida na STRESS zako. Mwisho ni ADHABU KWAKO pia.

Leave a Reply