Usiogope kuanza upya!

πŸ‘† Huo ni ujumbe wa Jacqueline Mengi siku ya leo!

Siku ya leo Jackie aliandika post mbili ya kwanza iliwakumbusha watu kua katika dunia hii ambayo unaweza ukawa kitu chochote kile basi chagua kua muungwana / mkarimu! “in a world you can be anything be kind”! Ni maneno machache lakini mazito sana! Sasa ujumbe wake wa pili ndio huo πŸ‘† halo juu, ambo wenyewe unawasihi watu waaiogope kuanza upya kwani hiyo ni njia ya FURSA mpya kwao na kufanya kile kitu ambacho roho yako ilikua siku zote inatamani!

Nikweli kabisa, usiogope kuanza upya eti kwasababu ulishindwa mara ya kwanza au maamuzi ya mara ya kwanza hayakuzaa matokeo uliyo tarajia! Niliupenda ujumbe bila kuwa na swali lolote kichwani mpaka pale nilipo kutana na post ya Faraja Nyalandu Murugenzi wa ‘Shule Direct’ mke wa Mh. Lazaro Nyalandu. Yeye aliandika ujumbe huu πŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎ

Mrs Faraja Kota Nyalandu

Reposted from @farajanyalandu May this new month remind you, you have all it takes to start and start again. That greatness awaits, that your little steps will lead you home. May you have eyes that see opportunities, a mind that seeks to build and hands that never destroy. May you overcome all that is holding you back. May you overcome you, if need be. May you find the peace to come back to the center of what truly matters. And find the Purpose that is above all. Happy New Month! – #regrann

Faraja ni kama alikua ametilia mkazo zaidi ujumbe wa Jacky! Naweza sema kama Jacky aliweka mbegu basi Faraja yeye akaweka mbolea na kumwagilia maji ili zao liote vizuri! Kwa kifupi Farajaja amesema tunapo anza huu mwezi mpya basi na uweze kukumbusha kuwa unacho kila kitu ambacho kinahitajika kuanza upya! Kwamba mambo makuu yanakungojea, hatua zako hizo ambazo ni ndogo ndogo zitakufikisha kwenye nchi ya ahadi! Basi na ukajaliwe macho yakuona FURSA mpya, fikra za kujenga na mikono ambayo kamwe haita bomoa! Na ukajaliwe ujasiri wa kushinda yale yote yanayo kukwamisha, na uishinde nafsi yako kama itahitajika kuishinda! Pia ukajaliwe amani ya kukuwezesha kutullia katika kile ambacho ni muhimu sana kwako na kuliko vyote!

Huo ujumbe wa Faraja Nyalandu ukaniwekea maswali kichwani mwangu! Je, Jacqueline Mengi anataka kuanza maisha upya?! Au hii ilitokea tu ujumbe zikagongana?! Wenye lugha zao wanasema “coincident”! Sina uhakika na maswali yote japo nimependa sana jumbe zote mbili kwani zina ujumbe mzuri sana wa kutia moyo!

Nachoweza kusema ni kua Jacky anaweza kufanya kitu chochote kile ambacho anatamani kufanya. Umri wake bado unamruhusu kufuta na kuanza upya! She’s too young kuvaa kofia ya “mjane”! Yes, mzee wetu kafariki lakini Jacky bado mbichi sana kukaa single! She needs a shoulder to lean on jamani! Anaweza omboleza mpaka pale atakapo jisikia yupo teyari kuanza familia mpya na mtu mwingine! Hilo halina ubaya kabisaaa! Ni baada ya muda gani; hiyo ni juu yake yeye kwani yeye ndio aliye vaa hivyo viatu anajua vinapo mbana! Ndio maana nikasema hawezi kukalia kiti cha mzee Mengi!

Jackie, wewe ukimpata Billionaire mwingine wewe tualike tu kwenye harusi sisi tutakuja bila shida 😍😍 na picha zako mie nitapost πŸ™ˆπŸ™ˆ Au ukijipatia mzungu fulani wewe tupe tu mualiko tutakuja! You are very free, and don’t let people victimize you kuvaa kofia ya ujane sijui kwa miaka kumi?! Nope! This is your “prime time” use it correctly!

Kikubwa wewe unabiashara zako nyingi tu zisimamie my dear ili siku watoto wako waje kuwa proud na wewe. Those little Billionaires (the twins) wana haki zote kwenye kila kitu ambacho kina jina la marehemu baba yao! Huu ni mtihani kwa Regina na Abdiel tuone kama watawatunza wadogo zao au la! Hao watoto ni jukumu lao kuwatunza kwa kila kitu! Yes, wewe mama yao upo lakini kama wataamua kuvaa viatu vya baba yao basi hao watoto ni jukumu lao kwa asilimia 100%! Mpaka watakapofika miaka 18 basi wapewe haki zao zote! Wao ndio wataamua nini cha kufanya! Na wakumbuke kuwa hao watoto wamezaliwa baba yao akiwa Billionaire teyari, hivyo hayo maisha ndio walio zaliwa na kuyakuta na ndio maisha wanayo yajua, hivyo hiyo ndio level ya style ya maisha tunayotegemea kuona wakiishi! Sisi wapembeni tutakua tunatizama kama kweli wana kee-up the standard! Huu utakua muda muafaka wa public kuwajua vizuri Regina na Abdiel ni watu wa namna gani kwa kutizama jinsi watakavyo wajali wadogo zao!

Kwakumalizia nasema, ndio unaweza kuanza upya nasi washangiliaji tutakua hapa kukushangilia! Unakila kitu cha kuanzia na kila sababu ya kuanza upya! Huwezi kuwa mjane forever! You are too young for that!

Leave a Reply