“watu wema wengi huishia kuwa na sifa ya UBAYA vinywani mwa watu lakini kwa kuwa MUNGU NDIE ANAELIPA!!”>>>> Zamaradi Mketema

Tenda wema unavyotenda, kuwa mwema unavyokuwa, mpende binaadamu unavyoweza, muoneshe kumjali kupitiliza, niamini kitu kidogo kitamsahaulisha yote makubwa tena hakuna ajabu kukuta kinachomfanya akuone mbaya ni haki yako, hakuna anaefanya jema kwa mtu ili alipwe, ila kuna ile hali ya KUONA na kuthamini juhudi anazofanya mtu ambapo hiyo inapokosekana ndio unakuta mtu unakuwa dissapointed kwa namna fulani, maana mara nyingine mtu unatoka hadi nje ya njia zako kumridhisha mtu ama hata kujinyima mara nyingine ili wengine wafurahi hata kama ni kwa kidogo, huenda ndio uwezo wako ulipoishia, lakini hakuna hisia mbaya na zinazoumiza kama kujihisi HUTOSHI ama huna unachofanya hasa kwa mtu ambae deep down unajua unafanya nini na unajali kiasi gani. Nilichogundua ukiwa mwema sana unaowafanyia mara nyingi wanakuonea, watakugandamiza, wata-take advantage of you na zaidi watavuka hadi mipaka yako mara nyingine hata kwa vile vitu vya kutumia tu akili, kiufupi watafanya hadi yale ambayo kihalali wasingeweza kuvumilia kufanyiwa na watu wengine na ukiongea ni KOSA, unakuwa mbaya, tena mara nyingine unaweza hata ukanuniwa, wanataka hata wanapokugandamiza unyamanze UKAE KIMYA hata kama ni haki yako kuongea. Ikikutokea usiumie na wala usiache kutenda pale inapostahili, watu wema wengi huishia kuwa na sifa ya UBAYA vinywani mwa watu lakini kwa kuwa MUNGU NDIE ANAELIPA!! Usiache kujitoa, uzuri yupo na ANAONA!!

Leave a Reply