Wema ni mwanamke dhaifu sana!

Siku ya jana ilikua ni siku ya wanawake dunia kote, kama ilivyokua kwa wengine basi naye Diamond alipost picha kuonyesha wanawake ambao ni muhimu kwake kama picha inavyo onekana hapo juu πŸ‘†πŸΏπŸ‘†πŸΏ na ujumbe wake! Hii nitofauti sana na tabia ya Diamond ambayo kwa miaka mingi amekua akiweka picha ya mama yake au saa nyingine anaweka na za dada zake.

Hakuna ubaya wa mtu yoyote kupost picha ya ‘X’ au ya “Ma_eX” zako kama bado upo single na unauhusiano mzuri nao. Lakini kwa hii ya Diamond inakua tofauti kwani inazidi kuonyesha jinsi gani Diamond anatabia za Unyanyasaji wa hisia (emotional abuse) kwa wanawake! Inazidi kuonyesha kua Diamond ni manipulator na narcissistic! Ukitizama wanawake ambao Diamond amekuanao kwenye mahusiano iwe kwa mapenzi yao wawili au bahati mbaya lazima utagundua na kukubaliana na mimi kua wote walijikuta wana poteza muelekeo wa maisha yao kusahau wao ni akina nani na nini wanataka kua katika hii dunia (they lost focus of who they are, their dreams, and what is their main purpose of existence in this planet world)!

Kaa chini angalia vizuri, utagundua kua karibia wote wanakua wakifanya vitu ambavyo vinampa Diamond ‘kiki’ ya kuongelewa na ku-boost muziki wake huku wao wakizidi didimia na kupauka! Anawatumia kutengeneza pesa lakini hawapi pesa za kufanya vitu vya maendeleo! halafu wao wenyewe wanakua hawashtuki mpaka watu wanapoanza kuwaonea huruma then wanadangwa na ‘maigizo’ ya kununuliwa gari na nyumba fake! Mtu ambaye alikua anaakili zaidi ya Diamond na alikua na uwezo wa kumshawishi Diamond kufanya vitu kwa maendeleo yake huku akijua kua 100% atanufaika na hayo maamuzi ni Zari the Bosslady peke yake na ndio maana familia haikumpenda. Na hii chuki ilianza baada ya kuweza kumshawishi Diamond anunue nyumba South Africa baada ya kuzaa naye Tiffah! Sidhani hata Tanasha kama ameondoka nalile gari la ‘maigizo’ ambalo alinunuliwa wakati wa birthday yake! Someone can prove me wrong, lakini naamini kwa asilimia zote limebaki Dar na sidhani kama lilikua kwa jina lake yeye Tanasha.

Kwanini nimesema Wema ni mwanamke dhaifu sana; wewe angalia katika huu ujumbe hakuna hata mwanamke moja ambaye ni Ex wa Diamond “kaushabikia” wala kujibu! Hila bidada hapa tobaaa! Embu soma comment yake hapo juu πŸ‘†πŸΏπŸ‘†πŸΏ Wema ngoja nikuulize, hivi kwalipi jema ambalo Diamond amekutendea mpaka awe na “special place” in your heart just for him?! Wanawake wengine wanajaribu kusahau hata majina ya “babydaddy” zao itakua Diamond?!

Huyu si ndio alikutumia wakati ukiwa upo juu, alipo ona thamani yako imeshuka akaenda zake? Kama hakukujali wakati ule upo mbichi leo hii umejizeekea kama akina Alpha hapa ndio atakuthamini?! Huyu Diamond juzi kati sialifanya sherehe ya miaka kumi tangu kuanza muziki, akawashukuru watu wote isipokuwa wewe! Wote walialikwa lakini wewe ukaachwa kama paka yatima! Sasa huyu mtu unawezaje ku reserve a special place in your heart just for him?!! Diamond anapenda attention na alifahamu fika kua kwenye hiyo sherehe angekuleta wewe attention yote ingehamia kwako, na hilo lisingewafurahisha ndio maana hukualikwa! Sasa inakuja issue ya Tanasha, Diamond alikua anajua hana mpango wowote na Tanasha ila hakujua kama Tanasha anaweza fanya maamuzi haraka hivyo imekuja kama surprise. Alijua angemchezea kama wewe! (Alisahau Tanasha ana damu ya Kijaluo, we are very intelligent! Tunajua kusoma alama za nyakati πŸ˜„πŸ˜„πŸ’ͺπŸ’ͺ) Sasa anataka kukutumia wewe kama ‘scapegoat’ kumuumiza Tanasha na kupata attention zaidi.

Wema, labda nikuulize kwanini unakubali kutumika kuumiza mwanamke mwingi?! Are you that insecure and miserable?! Kwasababu Only weak women ndio wana hiyo eager and energy ya kuumiza mwanamke mwenzio. Mwanamke anaye jiamini kamwe hawezi kukubali upuuzi kama huo! Mwanamke anaye jiamini kamwe huwezi mkuta anafanya vitu petty ili mradi apate attention! Mtu yoyote ambaye ana furaha yakweli toka moyoni kamwe hana muda wala nguvu ya kukera wengine.

Juzi kati nilikuona upo kwenye event ya Idriss Sultan nauliulizwa kama utakuja kufanya nae kazi ukasema ‘ndio’! sasa kwa mtaji huu unafikiri Idriss atataka kuinvest his money on you?! Who wants to take that “liability” girl?! Na hapa inawezekana hata Diamond amesikia dalili za Idriss kutaka kukunyanyua tena; hivyo katumia akili ndogo tu kukuzibia fursa! Kweli marehemu Mugabe alikuwa sahihi aliposema “If you a woman with beauty and no brains it’s your private part suffers most”!!

Mimi nafikiri unatatizo fulani psychologically, unahitaji msaada wa wataalamu! Na hakuna ubaya wowote kuomba msaada wa wataalamu kwani kila mtu anamatatizo yake na tunawaona hao wataalamu wanatusaidi. Kitu kikubwa na chakwanza kabisa ni wewe mwenyewe ukubali kua kweli ninatatizo, na wewe mwenyewe ukubali kua unahitaji msaada wa wataalamu wa Psychology hapo ndipo utakua umeamua kweli. Lakini bila kufanya hivyo utashangaa utakavyo zidi kuchezewa na hawa wanaume!

Diamond is an emotional and energy sucker person. Wabongo huwa wanapenda kuwaita “wanyonya damu”! Mtu kama Diamond ambaye ana tabia za kuweza manipulate hisia za watu na ni narcissist basi anakua na uweze wa ku drain your brain and your emotions mpaka unakuwa highly depressed, hapo ndipo atakupelekesha kama “msukule” vile. Kuwa makini sana na watu kama hawa, bila Mungu huwezi mshinda! Diamond akija kuoa ataoa for ‘cover-up’ lakini huyo mwanamke atakua anaishi kwenye ndoa yeye peke yake (married but no different with single women out there)! Yani anaweza akanunuliwa gari zuri, mafuta full tank 24 / 7 lakini harusiwi kwenda popote bila ruhusa ya Diamond. Kila kitu atakua anafanya just to shut people’s mouth na sio kwa mapenzi.

Anyway, hayo ndio yangu sina la zaidi. Nakutakia mafanikio mema!

Leave a Reply