Wonder woman!

Wonder woman ni nani? Je, wewe ni wonder woman?! Wimbo huu ambao umetungwa na mwanamke mwenzetu Zamaradi Mketema na kuimbwa na kaka Chris Lunda ili kuwahamasisha wanawake wasikate tamaa pindi wanapo anguka.

Ni wimbo unaovutia nankusisimua mno! Binafsi nimeusikiliza kama mara kumi hivi, lakini kil nilipo usikiliza nikama ndio nausikia kwa mara ya kwanza na unagusa hisia zangu zaidi na zaidi.

Wimbo huu umenifanya nirudi hapa kuandika kama ilivyokuwa huko nyuma, wale waliokuwa nami toka mwanzo wanajua jinsi nilivyokuwa natoa maoni yangu mbali mbali isipokuwa SIASA! Nilikuwa nataka kujaribu kuchukua likizo ya mwaka mzima ili niweke nguvu zaidi kwa swala fulani. Lakini huu wimbo kwa njia fulani unenipa nguvu zaidi ya kufikiria upya na kusema mimi ni “Wonder woman” Simba niliye mbugani natafuta mawindo hivyo siwezi kutafuta mawindo sehemu moja nikaridhika!

Ninawasomaji wangu ambao wameni miss sana, hivyo kutokuandika kwangu kuna waumiza! Hivyo nimeamu kusikiliza sauti ya mwanamke mwenzangu, my fellow wonder woman! Narudi tena, kwa nguvu zote! Mimi ni wonder woman hakuna kukata tamaa 💪💪
Zamaradi Mketema, TV host, Song writer (Wonder woman), Philanthropist

Ngoja niseme kitu ambacho huwenda wengine wanakiona lakini hawajasema hadharani. Katika viwanda vya habari na burudani kwa muda mrefu sana vimetawaliwa na wanaume, nafikiri sasa ni wakati muafaka wa wanawake wa Tanzania kuendesha hii industry!

Katika wanaume wote hawa ambao wanashikilia hii industry marehemu Ruge Mutahaba ndio alikuwa anaakili ya kuogopesha wengi! He was the brainer of all! Huo ndio ukweli! Lakini nikiangalia kwa wanawake, naona pamoja na mapungufu yaliopo kuna wakina Ruge wengi tu kama tukiamua kushikana mikono na kusimama pamoja!

Kuna wanawake wengi sana nawaona wenye uwezo wa kufanya makubwa sana kama mtaacha hizi “pettiness” ambazo zinaleta mgawanyiko kati yenu! Ni wakati sasa waku-stop these “bullies” in media and entertainment industry! Sisi ni wonder woman hatushindwi!

Leave a Reply