Zamaradi Mketema: Kama unaweza kupokea machungu yangu bila kunihukumu kwanini ushindwe kuibeba furaha yangu bila kunituhumu

Dunia ya sasa ni dunia ambayo watu hawataki wala kufurahia kuona unasherehekea mazuri yako, na unapofurahia inatafsiriwa kwa namna tofauti na kila mtu atakuangalia kwa jicho lake. Wanachoona sawa ni post za malalamiko na kutamani kila siku upost huzuni zako wakupe pole kitu ambacho sidhani kama ni sawa. Tusichofahamu kila mtu ana kitu kinachompa raha ama satisfaction, tupeane nafasi na uhuru wa kufurahia bila kuhukumiana vile vinavyotupa furaha kwenye maisha. 

Kama unaweza kupokea machungu yangu bila kunihukumu kwanini ushindwe kuibeba furaha yangu bila kunituhumu, maana tunatakiwa kufurahia kila hatua hata kama ni ndogo kiasi gani sababu hatujui hizo kubwa tutafika lini. Tuache watu wafurahi, tunavyopokea aibu zao basi na ushindi wao tuupokee, sio kila kitu tukitafutie namna ya kukichafua na kuona kama unaoneshewa wewe, hata MUNGU hupenda kushukuriwa na sio malalamiko kila siku bila kuangalia Baraka nyingine. Sasa pia kwenye maisha ya kawaida kwanini tuoneshe yanayotupa tabu tu bila kugusa na yanayotupa furaha pia, unapofurahia kitu utasikia watu wenye roho za kichawi "na ukifeli/ukianguka pia utuoneshe!!"  
Jamani KUANGUKA KUPO TU ni sehemu ya maisha, na ndio huko kunakotufanya tufurahi tunaposhinda. Tunafurahi kwa kipindi hiko na kushukuru, hakuna ubaya wa kufurahi pia tunapopata, na ukimuona mtu anafurahia ushindi wake muache, tusilimitiane na kuhukumiana, hujui kwake ina maana kiasi gani ama amepigana kwa namna gani, ama ameomba MUNGU mara ngapi kufikia hapo, hata kama kwako ni kawaida. Tumeagizwa kufurahia na kupokea nyakati zote, so usisubiri mpaka upate kubwa ndio usherehekee, ENJOY THE MOMENT, ya mbele anayajua MUNGU.

 

Leave a Reply