Zamaradi Mketema: Karibu tarehe 15th April ukumbi wa MAKUMBUSHO YA TAIFA

Regrann from @zamaradimketema  -

Tumejikuta tunatambua wanawake wengi ambao wamefanikiwa leo hii na kuwaangalia kama watu waliozaliwa wakawa tu hivyo walivyo kutokana na picha yao ya leo bila kujua struggles zao, machozi yao, mapito yao, kusota kwao, kushindwa kwao, kufeli kwao, kukataliwa kwao na hata mateso na changamoto nyingi zilizofunikwa na HALI ZAO ZA SASA.

Katika safari ya maisha na utafutaji wengi huangalia CAPITAL kama ufumbuzi ama kitu pekee kinachotukwamisha kusonga kwenye NDOTO tulizonazo bila kujua kuna vingi huwa vinaturudisha nyuma wanawake na huenda ni matatizo makubwa kuliko kukosekana kwa capital ama vianzio, na hivyo vitu ndio vinafanya hata uwe na kazi ushindwe kuifanya ipasavyo ama hata kuichukia mara nyingine, ama kuna muda ujione huna tu thamani na kukufanya uogope na kunyong'onyea hata pale unapotakiwa kujitokeza na kutoa ulicho nacho, ama ushindwe kusimama vizuri kwenye biashara yako au kushindwa kabisa kuanzisha chochote kutokana na mengi yaliyokuelemea.

Huenda kwasasa uko kwenye hii STAGE, na kuhisi mbele hamna maisha, jambo moja unalopaswa kujua ni kwamba HAWA WANAWAKE UNAOWAANGALIA KAMA MIFANO wengi wao wamepitia kwenye hatua ambazo upo sasa, kuna ambao waliwaza hata kujiua, kuna ambao waliwahi kukosa kabisa, kuna wale waliopoteza dira kiasi cha kutokujua cha kushika, na kuna kipindi walijiona hawana thamani kama ambavyo UNAJIONA SASA, lakini hawakukubali, WALIAMKA, na wakagoma kupelekwa na upepo huo, wakasimama imara na mpaka leo hii tunawapongeza na wengine kuwaita ROLE MODELS. 

Hivyo hata kwako, kwa hali yoyote unayopitia sasa, nataka nikwambie INAWEZEKANA!! nakuahidi utavuka na utaipita hiyo hali na kuwa mpya kabisa, na hakuna ajabu kesho tukakutolea reference kama mmoja wa mifano bora ya wanawake waliofanya maajabu.

Amka kwenye huo usingizi, sio wewe peke yako unaeteseka, na hata kama unapitia manyanyaso, vikwazo, kutokuwa na Dira ya maisha ama changamoto yoyote iwe ya Kijamii, kihisia ama KIUCHUMI nakuhakikishia una nafasi kubwa ya kutoka huko na KUSIMAMA IMARA.

Karibu tarehe 15th April ukumbi wa MAKUMBUSHO YA TAIFA POSTA opposite na IFM kwa mengi zaidi, 

The GOAL is to change LIFE. Na hii siku itakuwa mwanzo wa safari ya mafanikio kwa WENGI. NI BURE!!!  - #regrann

Leave a Reply