Zamaradi Mketema: Katika kipindi cha Dawa usikimbie Dozi, na wala usilaumu mtu kwa ugonjwa wako

Regrann from @zamaradimketema - Kabla ya kupona kila mtu lazima apate Dawa yake, nyingine huwa chungu, nyingine tamu lakini ndio DAWA. Kwa bahati malengo ya dawa si mabaya ila kukusimamisha tena, kukufanya uogope ugonjwa ulioumwa ili uepuke vyanzo vyake, kutahadharisha na wengine waepuke sababu unajua uchungu wa matibabu yake, kwenye maisha DAWA tunazipata kupitia MATOKEO ya matendo yetu, yale tuliyoyatengeneza ndio yanatupa majibu yake, kwenye dawa hapa unaweza kudhalilika, kuumia, kutaka hata kujiua, kushuka thamani na vingi vingine, kutegemea ukubwa wa ugonjwa wako na ndio Dozi itakavyoenda, lakini uzuri ukishatambua unachoumwa na kukubaliana na hali bila kusahau kufata masharti ya ugonjwa unavyotaka unapona tu na mwisho wa siku maisha yanarudi kuwa mapya. Katika kipindi cha Dawa usikimbie Dozi, na wala usilaumu mtu kwa ugonjwa wako, pambana nao mpaka usimame upya, kiufupi usiyakwepe masharti maana kipindi cha Dawa ndio kipindi cha kujifunza, jua tu SIO PEKE YAKO mwenye ugonjwa huo, kuna wengi walioamua kuugua kwa siri ama kuficha matokeo yake tumewazika, kataa kuondoka na gonjwa lolote, ujinga ni wakati wa kwenda hivyo kikubwa jifunze athari zinazoweza kusababishwa na matendo yako, na kupona kwake ni kutotafuta yeyote wa kumuangushia mzigo wa lawama ila kuangalia mianya uliyoitoa iliyosababisha ugonjwa kuingia, kisha chaguo ni lako kuidhibiti ama kuachia nafasi ya ugonjwa kukushambulia kwa mara nyingine. - #regrann

Leave a Reply