Zamaradi Mketema: Namshukuru kwa yote yaliowahi kutokea kwenye maisha yangu….!

Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru wote waliotenga muda wao kwa mapenzi kabisa kunitakia heri katika siku yangu ya kuzaliwa, kwa kila alieniwish hata kama sijaona nataka utambue NATHAMINI SANA SANA SANA, MUNGU awabariki kwa upendo wenu kwangu na asanteni sana kwa Dua njema Birthday ya mwaka huu kwangu ni kubwa mno na yenye Baraka nyingi, nitakuwa kiumbe wa ajabu kama SITAMSHUKURU SANA MUNGU kwa mengi aliyoyatenda kwenye maisha yangu, hii sio akili yangu, wala sina maarifa ya kuzidi wengine ila huyu ni WEWE MUNGU WANGU. Namshukuru kwa KUNISHIKA MKONO, namshukuru kwa KUNIONGOZA, namshukuru kwa KUNISIMAMIA, namshukuru kwa KUNILINDA NA KUNIPIGANIA, na namshukuru kwa yote yaliowahi kutokea kwenye maisha yangu haijalishi kwa wengine yalikuwa na sura gani lakini naamini mengi ni ngazi ya kunifikisha nilipo. Naendelea kujikabidhi na kukabidhi kila kilicho changu mikononi mwake na kumuomba aendelee kunilinda na kunilindia maana mimi kama binaadamu sina ninachokiweza. Bila kusahau wazazi wangu waliotangulia mbele za haki, Zamaradi wa leo ni taswira yenu, asanteni kwa malezi yenu na asanteni kwa kila MLICHOKIPANDA kwangu, Nawaombea kwa MUNGU aendelee kuwapumzisha kwa amani na awape makazi yaliyo mema INSHA’ALLAH Na kwa kila mwenye mapenzi mema, ndugu, jamaa na marafiki wote mfahamu NAWAPENDA NA ASANTENI SANA SANA.

Leave a Reply