Zamaradi Mketema: Ni Makosa yetu wanawake

Miriam Kinunda author of  Taste Of Tanzania: Modern Recipe for the West https://www.instagram.com/miriamkinunda/

Regrann from @zamaradimketema -Kwenye comments nimegundua wanawake wanalalamika na mzigo wanaoubeba wao kwenye majukumu ya familia, ila MAKOSA mara nyingi yanaanzia kwetu, wanawake wengi WANAWALEMAZA sana wanaume wao wenyewe kwa kuhisi wanawasaidia, kwa bahati mbaya hii haina faida kubwa mbele ila hasara.

Tukirudi kwenye nature mwanamke ameumbwa kutunzwa hata vitabu vyote vya Dini vinasema hivyo, na ndiomana ikiwa tofauti madhara tunayaona, mwache mwanaume awe mwanaume hata kama umemzidi kipato, nature ya mwanaume ni KUTOA na kujihisi ANAMILIKI na ndio uanaume wake unapokuja, anapokutunza anafeel uanaume wake, hata uwezo wa kunguruma anaupata ndani, mpe hiyo nafasi usimnyime, hata kama wewe una mia yeye ana kumi hakikisha katika kumi yake lazima utaratibu wake wa kulisha nyumba ubaki palepale kwa kidogo chake hikohiko, we utatumia tu akili jinsi ya KUMSAIDIA ila usimlemaze akaona wewe ndio kilakitu na kumpa nafasi ya kutulia, hakikisha kila anapotoka anaacha kinachostahili hata kama ni mia tano, mfanye awe mume, maana athari za wewe kuibeba familia mara nyingine zinaenda pabaya zaidi hadi kuharibu mahusiano.

Na ndiomana kuna fikra isiyo rasmi kuwa wanaume wengi wanaoishi na wanawake wenye uwezo zaidi yao hutafuta nyumba ndogo pembeni za hali ya chini na kuzihudumia kwa hikohiko kidogo, lengo ni kutaka kuutoa uanaume wake, anataka mamlaka yake yaonekane, anataka akiongea asikilizwe, mpe nafasi hata kama una uwezo, hiyo ndiomaana ya kuwa KICHWA mfanye awe kichwa kwa vitendo, hata kwa umasikini wake onesha unamtegemea yeye na umtie moyo afanye kadiri ya uwezo wake, sio ndio unazo basi yeye anakuwa kama mtoto mdogo sasa ndani unamuacha moja kwa moja hapana, au unajifanya huhitaji kitu kwake unakosea. Ukitaka kujua hii ni nature hata kwa upande wa wanawake ndiomana hakuna feeling nzuri kama kupewa/kutunzwa na mwanaume wako hata kama una kilakitu, sababu nature iko hivyo!! Ndiomana si ajabu kukuta mwanamke tajiri lakini akamtamania mwenzie wa hali ya chini kwa kununuliwa mkufu tu, pamoja na kupata kilakitu kwa jasho lake bado kuna kitu kinamiss, kuona mtu anasimama kwake kama MLINZI na mtunzaji wa maisha yake, MUNGU ndio kaumba hivyo!! Ila siku hizi eti wanaume ndio wanalindwa. Ni Kosa!! Regrann from Zamaradi Mketema

Leave a Reply