Nawatakieni Mwaka Mpya mwema!

Screenshot_2015-12-07-19-41-52-1Wapendwa wasomaji wangu, ndugu, jamaa na marafiki. Napenda kuwatakieni kheri ya kuufunga mwaka 2015 na kufungua mwaka 2016. Nasema asanteni sana kwa kutembelea hii blog bila kuchoka, sina cha kuwalipa zaidi ya asante. Naomba mnisamehe wale wote niliyo wakwaza kwa namna moja ama nyingine. Sidhani kama nilikusudia kumuumiza mtu na sina huwakika kama nimemuumiza mtu yoyote! Lakini kama binadamu huwezi jua hivyo najishusha kwa kusema I am sorry! Tuzidi kupendana, tuombeane, na tutakiane mema siku zote! ……………….Mdogo wangu ? Blessing naye anawatakieni mwaka mpya mwema. Anasema yeye ni mpenzi wa hii blog hivyo siku zote anatembelea na kuwasoma hapa kwa kutumia mtandao wenye mawasiliano na Internet ya kuaminika. #Halotel ndiyo habari ya mujini na vijijini!

Nawaacheni na huu wimbo. Nimoja ya nyimbo ninazo zipenda sana sana. Yani huwa nausikiliza kwenye gari karibia kila siku!

Happy New Year wapendwa. Tukutane 2016 ???

Wimbo nilio upenda zaidi mwaka huu 2015 #Utanipenda?

Screenshot_2015-12-19-18-45-35-1-1Nimeusikiliza huu wimbo zaidi ya mara 20, believe me! wimbo huu una ujumbe mzito sana ambao mtu yeyote yule anayekaa chini na kutafakari vitu haswa watu walio kuzunguka lazima utakuliza! Very touchy song with a Billion $$ question #Utanipenda? Nakuletea behind the scene za wimbo huu na wimbo wenyewe angalia na tafakari sana tunapo malizia mwaka huu na ufanye maamuzi sahii! Je hao watu iwe ni rafiki, jamaa,  wapenzi, n.k waliokuzunguka je ungekuwa hauna hivyo vinavyo wavutia sasa je wangekubali kusimama nawe? Je vipi vikiondoka ghafla wataendelea kuwepo au nao wataondoka? #Utanipenda? Screenshot_2015-12-31-13-36-19-1

#TBT# Mahojiano yangu yamwisho kwa mwaka 2015: Bin Zubeiry

FB_IMG_1437541501275
Najua mimi na wewe tunafamiana toka tukiwa wadogo lakini kwa faida ya wasomaji naomba ujitambulishe maji
na yako halisi:  Asante, mimi ninaitwa Mahmoud Ramadhan Zubeiry,   walizoea kuniita Mudi
Unaweza ukatuelezea kidogo kuhusu elimu yako?  Shule ya msingi nilisoma pale Mgulani, baadaye nikaenada Rutabio sekondari kabla ya kufanya kozi mbili za awali za Uandishi wa Habari MAMET (Maarifa Media Trust), chuo ambacho kilikuwa kinamilikiwa na akina Jenerali Ulimwengu. Baada ya hapo, mwaka 2008 nilipata Stashahada ya Uandishi wa Habari ya LSJ (London School of Journalism) ambayo nilifanya online
FB_IMG_1437541539371
Ilikuwaje mpaka ukaanzisha blog yako na kwanini uliiita binzubeiry?
Baada ya kufanya kazi za kuajiriwa kwa muda mrefu tangu mwaka 1999, katika magazeti ya Dimba, Mtanzania, Rai, Bingwa, The African na baadaye Tanzania Daima na Sayari hapa nyumbani nikaona sasa inatosha. Lazima nisimame kama mimi kutafuta mafanikio binafsi. Ndipo nikaamua kuanzisha blog, ambayo sasa imekuwa tovuti kamili ya michezo, www.binzubeiry.co.tz
FB_IMG_1437541634585
Yalikuwa maamuzi magumu, ambayo mpinzani wa kwanza alikuwa mke wangu, pale nilipomuambia ghafla ninaacha kazi mwaka Mei mwaka 2012. Kama unavyojua mishahara ya kwenye vyombo vya habari hapa nyumbani haitoshelezi kukidhi mahitaji- hivyo niliacha kazi sina chochote. Sikuwa hata na kiwanja. Nilianza blog katika mazingira magumu sana, sina vifaa, nahangaika kusaka habari mitaani. Nilijituma hivyo hivyo hadi blog ikaanza kuvuma hatimaye nikaanza kupata watangazaji, taratibu nikaanza kununua vifaa vya kazi. Alhamdulillah sasa nina vifaa ambavyo ninafurahia kufanyia kazi, kuanzia kamera, MacBook na zagazaga zote. Nipo full, ila tu ofisi bado popote.
FB_IMG_1437544009848
 Hali ikoje leo? Alhamdulillah ninamshukuru Mungu, watoto wangu wane kati ya watano wote wanasoma shule za kulipia, wawili kati wao sekondari kidato cha kwanza (Nurat na Precious). Wawili wapo shule ya msingi darasa la kwanza (Prince Akbar) darasa la pili (Princess Asia). Mungu akijaalia mwakani Sheikh Yussuf (miaka miwili) ataanza chekechekea. Nina shamba la embe ekari mbili eneo la Kigamboni. Nina nyumba Kigamboni huko huko na kiwanja ambacho hakijajengwa bado cha ukubwa wa 40-40. 
FB_IMG_1437543931792Unamagari mangapi? Yapo matatu tu, Passo anayotumia mke wangu, Range Rover na BMW ambazo natumia mwenyewe
Inaelekea unapenda sana michezo, je ulisomea uwandishi wa habari upande wa michezo au ni kipaji tuu ulizaliwa nacho?
FB_IMG_1437544757337
Kama utakumbuka napenda michezo tangu nipo mdogo, nimecheza mpira mwenyewe pale KJ, lakini sikubahatika kufika mbali. Wakati nipo shule ya msingi Mgulani nilichaguliwa na Mwalimu Chale kama unamkumbuka katika kikundi cha Chipukizi, ambao ndiyo tulikuwa Ball Boys wa Uwanja wa Taifa enzi hizo mpira wa Tanzania uko juu sana. Kwa hivyo tangu hapo nikawa mpenzi sana wa michezo. Kwa kupenda kusoma magazeti, nikapenda sana na mimi siku moja niandike. Nilikuwa navutiwa wana na uandikaji wa watu kama Johnson Mbwambo na Francis Chirwa. Nilitamani siku moja niwe kama wao. Nashukuru walikuwa mabosi wangu, walinifundisha kazi katika gazeti la Dimba kwa upendo kabisa. Kama ninasifiwa leo ni Mwandishi mzuri wa michezo, basi kwa sababu nilipitia kwa walimu wazuri hao na wengine wengi kweli. Eric Anthony alikuwa Mhariri wangu wa kwanza pale Dimba. Huyu jamaa alinipiga msasa sana.
FB_IMG_1437544685611Ulipata wapi ujasiri wa kuanzisha blog yako mwenyewe?haswa ukitazama hapo nyuma watanzania walio wengi walikuwa wanafikiri kuanzisha blog ni lazima uwe mtu maharufu au mtu ambaye umetoka kwa familia yenye pesa? Kama nilivyokuambia, niliamua tu kujilipua kwa kuacha kazi na kwenda kujiajiri mwenyewe. Nilijikabidhi kwa Mungu na leo ninamhsukuru sana Mungu kwa kweli. Amenisamamia na anaendelea kunisimamia. BIN ZUBEIRY ndiyo habari mjini
Hii blog unaitumia kama sehemu tuu ya vitu unavyo vipenda au pia ni sehemu ya kujiingizia kipato? Mama hii ofisi, inafanya niishi kupitia malipo ninayopata kutokana na vijitangazo hivyo. Ukiondoa hii tovuti, mimi mkulima na nina mpango kuanza mradi wa ufugaji nitakapohamia kwenye nyuma yangu Januari Mungu akipenda.
FB_IMG_1437541894205
Najua watu wengi hawajui historia ya ulipo tokea ila kwa sisi tulio kufahamu tunaona ni ukuu wa miujiza ya Mungu. Je wewe ulisha wahi kuwaza wakati wa utoto wako kuwa ipo siku moja utaishi maisha haya unayo ishi sasa hivi? Labda udokeze kidogo maisha ulio kulia: Kuna wakati huwa nalia mwenyewe ninapokumbuka nilipotoka, misukosuko na shida za maisha nilizopitia. Lakini mwisho wa siku ninamshukuru Mungu tu, kwani yeye ndiye mpangaji wa yote. Niseme nini Alpha, mimi nimetokea familia ya kimasikini pale Keko wewe mwenyewe unajua. Tulikuwa na maisha duni kupita duni zote. Kuna wakati nilikuwa nakwenda kwenye jalala la soko dogo pale Keko kuokota vilivyotupwa na kutafuta vyenye nafuu ili twende nyumbani kupika kupata chakula. Nilianza kufanya deiwaka hata kabla sijaanza darasa la kwanza, napimisha watu uzito kwa mzani si unakumbuka? Na ni ule mzani ulinosomesha mimi, ilikuwa kila nikitoka shule naenda kusanya, Napata fedha za mahitaji ya shule. Nilikuwa nakwenda kubeba mizigo Kitumbini. Nimepiga debe, nimeuza mitumba minadani. Manyanyaso, chuki na masimango hivyo ni vya kawaida.
2Wewe ni mtu au mwandishi wa habari pekee ulie bahatika kuona gari la kifahari (ambalo ni custom made) la kijana wa Bhakresa; ulijisikiaje ulipo pata fursa hiyo? Kwanza mlifahamiana wapi au ulimjuaje?
6
Yussuf ni rafiki yangu. Tumejuana kutokana na kazi, wao wanamiliki timu ile ya Azam FC. Alipenda ninavyoandika habari za timu yao, akawa rafiki yangu, tumeshibana hadi tumeaminiana kiasi hicho.
5
Na Yussuf pamoja na Zacharia Hans Poppe ni watu wenye mchango mkubwa katika maisha yangu. Hawa ni wafadhili wakuu wawww.binzubeiry.co.tz
8
Ni nini umejifunza zaidi au faida kubwa umepata kutokana na mitandao? Je unafikiri watanzania wanatumia vizuri mitandao?
Nimejifunza mengi sana, nilisahau kukuambia, nilisoma kozi moja fupi pia ya namna ya kuendesha blog mwaka 2012 ilidhaminiwa na SBL (Serengeti Breweries). Kuhusu matumizi, si Watanzania, watu dunia nzima wapo wanaotumia vibaya mitandao ya kijamii. Na vigumu kuwabadilisha. Hizo ni hulka. Mtu anayejishimu hawezi kuposti picha za ngono. Hawezi kutumia mtandao kumtukana mtu.
FB_IMG_1437541501275Nini ujumbe wako kwa Watanzania wenzako? Ujumbe wangu kwa Watanzania na vijana wenzangu. Wamtegemee Mungu, waache ushirikina. Mafanikio yanakuja baada ya kujituma. Lazima tufanye kazi, tuache majungu. Tanzania itaendelea zaidi, iwapo vijana watafanya kazi kwa bidii.

Continue reading #TBT# Mahojiano yangu yamwisho kwa mwaka 2015: Bin Zubeiry →

A word of wisdom

Dr. Ben Carson (Retired world renowned neurosurgeon, and Republican Presidential Aspirant) wrote this beautiful piece. Read and be blessed……… FB_IMG_1451232210742

“Sometimes you are unsatisfied with your life, while many people in this world are dreaming of living your life.

A child on a farm sees a plane fly overhead and dreams of flying. But, a pilot on the plane sees the farmhouse and dreams of returning home. That’s life!! Enjoy yours.

If wealth is the secret to happiness, then the rich should be dancing on the streets. But only poor kids do that.

If power ensures security, then officials should walk unguarded. But those who live simply, sleep soundly.

If beauty and fame bring ideal relationships, then celebrities should have the best marriages. But those who live simply, walk humbly and love genuinely!

All good will come back to you!!!

Man asks, “Where was God when Myles Munroe, wife and his associates were killed in a crash? He answers, “The same place I sat when John the Baptist my servant was beheaded. When Stephen my servant was stoned to death. When Paul my servant was murdered in Rome. The same place I sat when my only Son was brutally crucified, wounded, bruised and killed. I have not moved from my position.” I am the same. It is not the means of exit from earth that matters but the destination. Live simply. It’s all about God!!”

kheri ya siku ya kuzaliwa mdogo wangu Guka Igogo

FB_IMG_1451527333377Oya! Siunajua nakupendaga right ? Ok. Nakutakia furaha na kheri ya siku ya kuzaliwa kwako. Mungu akuzidishie neema.  FB_IMG_1451544121654May u have more faith in God as u turn……years old! All I can wish u on ur birthday is happiness, success and long Life in this world my adorable baby brother Guka Igogo….I Love u  n u know it aah! (Your sister ☝) FB_IMG_1451527512623Happy birthday dogo and Prosperous New Year ?❤

Happy birthday Hon. Madam, Judge

FB_IMG_1451549312362

My heartfelt birthday wishes to my darling cousin-sister Honorable, Madam, Judge Dr. Modesta Makopolo! Wishing countless blessings filled with joy, love, and happiness.  Happy birthday mutoto wa shangazi yangu. Love you! ?

Kheri ya siku ya kuzaliwa mdogo wangu Mai Igogo

FB_IMG_1446522356989-1Kheri ya siku ya kuzaliwa mrembo wa Utegi ? uwe na mwaka mpya mwema ulio bubujikwa furaha na amani. Happy birthday beautiful! Love you!

Kheri ya siku ya kuzaliwa Mwl. Ngonyani

20150704_181835-1Nakutakia kheri ya siku ya kuzaliwa mzee wangu Mwl. Ngonyani. Mungu akulinde, akupe afya njema, na furaha tele. Pia uwe na kheri ya kumaliza mwaka 2015 na kuuanza mwaka 2016. Ubarikiwe siku zote. Much love from Texas.

Eddah Elegant Catering Christmas party

FB_IMG_1451545129314

Niliahidi kuleta hizi picha hapa, basi ngoja nitimize ahadi yangu. Kwa wale mliotukutia kati ni vihi, wiki iliyopita siku ya Christmas Eddah Elegant  Catering iliandaa party kwa familia na wanajumuiya wote wa ishio Maryland na vitongoji vyake. Basi zifuatazo ni picha za kazi waliyoifanya. IMG_3108+(2)Huyu ndio mama EEC (Eddah Elegant Catering) mwenyewe. Hongera sana tena sanaaaaaa Eddah Gachuma.  Kazi yako imefurahiwa sana. Nawewe  mwenyewe ulipendeza sana.FB_IMG_1451545162405FB_IMG_1451545249998Mapambo na rangi zake zimeendana kabisa na tukio. Imependeza sana. FB_IMG_1451545120887Ninaposema Eddah Elegent Catering naomba ujuwe kuwa si wababaishaji ati! Ni watu wa huwakika na kile wanachokifanya. Hivyo usije sita kuwatumia pale unapo hitaji catering. FB_IMG_1451545136241Nimependa Ubunifu wako wakujua kuwa Christmas ni siku ya kifamilia zaidi hivyo ukakumbuka kuweka sehemu ya watoto nao wakafurahi. FB_IMG_1451545155999Unajua hakuna ubaya wowote watu hata kumi kufanya biashara ya aina moja. Kitu kikubwa ni ubunifu! Wewe unajitofautishaje na wengine ili uvutie wateja wote kwakoFB_IMG_1451545148021 Kwa mfano kuna weza kuwa hata na KFC kumi katika eneo moja lakini huduma zao ndizo zitakazo watofautisha kati ya mmoja na mwingine. FB_IMG_1451545099006Hivyo kazania sana kuwa mbunifu, na huduma zako zidisha ubora zaidi ya hapa. Hata kama unapata faida kidogo lakini kama watu wanakupenda watakuita kila siku kwenye sherehe zao. Ukishajenga trust kwa wateja wako yani hata uwa charge kiasi gani watakuita tuu. FB_IMG_1451545243722Kwa mara nyingine tena hongera sana Eddah Elegant Catering kwa kazi nzuri unayofanya. Najua next time itakuwa nzuri  zaidi na zaidi. IMG_2962Wapendwa hizi ndizo party za kwenda haswa kwa wazazi. Party zenye heshima na hadhi zake . Party ambayo uwoni aibu kumwambia mtoto wako twende sote mwanangu! Party ambazo zinajali familia na kuandalia watoto sehemu yao bila gharama ya ziada. Siku nyingine ukisikia EEC  wanaandaa event yoyote yani usikose. FB_IMG_1451545175317

Hot shot of the day

FB_IMG_1451413399069Wow! Black Beauty! Huyu anaitwa Aisha toka Bongoland. Nimependa sana hii picha, haswa ngozi yake. Ngozi nyeusi laini na nzuri kabisa. I mean her skin texture is to die for! Mimi binafsi napenda sana weusi wangu tatizo nililonalo; ngozi yangu ya uso inamafuta sana hivyo huwa napata chunusi usoni. Na dawa nyingi za kuondoa chunusi zina bleach basi napataje shida?! ?? kwa hiyo huwa nikiona watu wenye ngozi kama ya Aisha huwa na furahia sana. Tunza ngozi yako dada ni rangi adimu sana kupata sikuizi. Nashukuru sana Mungu mwanangu naye anangozi kama yako, very soft!Ubarikiwe sana mpendwa. Uwe na mwaka mpya mwema.

Happy 61st birthday Denzel Washington

FB_IMG_1451413073598Awii! Nampendaje sasa huyu mwanaume  ?? mwanaume mwenye akili timamu zilizo kamilika, mcheshi, mnyenyekevu, ana wingi wa hekima na busara, aliye jawa na hofu ya Mungu! Did I say he got money too?!?? Mh!  some women are just lucky huh!??  quote-goals-on-the-road-to-achievement-cannot-be-achieved-without-discipline-and-consistency-denzel-washington-86-37-902adefaf6af75a60bdeaaa856016f86c4tumblr_nf935igPKG1rj4ktlo1_1280twjf3dg9x0hrizfia5ldqpi1pyeceqwg7hllk0rzdhbbpl0jffjhyc3tqoiqauog61 and still hott! Happy 61st birthday Mr handsome! God be with you always ❤

Kutoka Facebook

FB_IMG_1451412986552Leo kutoka Facebook nimependa sana hii picha ya Zawadi na binti yake. Wao wameenda kupumzika huko Bangkok kwa sasa. Unaweza wa follow kwenye IG kwa majina haya Zawadi Kakoschke, Bintimalaika, au wa tembelea kwa familia blog yao hii www.maisafari.com

Happy birthday Sophia Makoyo!

FB_IMG_1451407967067Napenda kumtakia my darling cousin-sister kheri ya siku ya kuzaliwa. Ubarikiwe sana, uwe na maisha marefu yenye amani, furaha, na afya njema. Mungu akutangulie katika masomo yako. Happy birthday girl! Much love ?

“Tumtangulize Mungu we are nothing bila Mungu”

Screenshot_2015-12-29-11-05-36-1

12362620_449315031941575_1991418514_n

Mother and daughter moment

Screenshot_2015-12-29-01-24-00-1Kichuna cha Kizaramo a.k.a Missy LB muke ya Mali pamoja na binti yake kipenzi Brenda. Napendaga sana hii familia na smile zao, lovely and genuine!? Wamependeza sana. Mbarikiwe wapendwa.

Happy birthday Vincent

FB_IMG_1451356048279-1Kheri ya siku ya kuzaliwa shemeji yangu Vincent. Nakutakia maisha mema, marefu, yalio jaa upendo, amani, furaha, na afya njema. Ukazidi kuwa na busara na hekima ya kuitunza familia yako na mkeo kipenzi. Zaidi ya yote ukapate kuwa karibu na Mungu wako zaidi ya jana. Bila Mungu vyote ni batili! FB_IMG_1451356105461-1Mweee! Eddah mtoto ya Gachuma Muke yake na Vincent, dada yangu umelamba “dume”au dume limekulamba ?? what a lucky man with a blessed lady on his left shoulder! Da Eddah enjoy your blessing my dear ? wa namna hiyo ni wachache sana ! FB_IMG_1451356007425Unaona wapendwa, ukishafika umri fulani na unafamilia nyumbani inakutegemea  hivi ndivyo unataka kufurahia sherehe yako ya birthday;  Small party / gathering  na watu fulani amazing wanaojitambua ? safi sana ? classic! FB_IMG_1451356084539Jamani kujitambua ni muhimu sana. Vitu kama hivi havifanywi na watu wasio jitambua! Yani utakuta baba zima mwenye watoto kutwa yupo bar au kwenye nyumba za mwanaume wenzake eti “chilling na mshkaji” sasa huyo “mshkaji” anakushika nini mpaka ushindwe ku chill with your family?! #SMH Sehemu kama hizi mnakutana na ku have fun kwa masaa kadhaa kisha kila mtu anaondoka zake home. Hongereni kaka na shemeji zangu kwa kujitambua. FB_IMG_1451356022836My wii Lulu wa Saria na dada yangu Eddah wa Vincent mmependeza sana ? FB_IMG_1451355954025So beautiful. Pendeza sana ladies. FB_IMG_1451355936617Eee dada Eddah  eeh!  Tuambiane basi nini siri ya hili penzi?! ??  wenyewe wa “mujini” wanasemaga “kizuri kula na nduguyo” sasa mbona wewe unakula pekeyako ?? haya bwana……….Vincent’s face expression speaks volume! tena kwa maringo na mikogo yote , just love it! FB_IMG_1451355985418-1Happy birthday Vincent.  Na asante kwa kunitunzia dada yangu. Ubarikiwe sana.

Hot shot of the day

FB_IMG_1451319250202-1Gorgeous Alicia kutoka Kansas state. Mimi napenda sana watoto ambao hawapakwi pakwi makorokoro usoni au kutengenezwa nywele kama wanawake wazima. Let kids be kids jamani. Tuwafundishe watoto kujikubali na kujipenda kwa jinsi walivyo. Inasaidia sana kukuza their self-esteem na confidence wanapokuwa wakubwa. Hongereni sana wazazi wa Alicia kwa malezi bora. Mbarikiwe sana.

Dada wa Taifa la Tanzania katikati ubora wake!

FB_IMG_1451317257396Naomba nianze kwa kusema hivi, msinichoke kumuweka au kumuongelea huyu dada yangu kipenzi cha roho yangu ndani ya hii blog! Naomba muelewa nampenda sana kwani ni wapekee mno! Usije ukafikiri ni kwasababu ni “super star” ndo maana na muweka humu hapana ni roho yake ya ukarimu, utu, na uungwana wake ndio maana na muweka humu and freely with all my heart I will always  support what she’s doing. Watu kama dada ShyRose Bhanji ni wachache sana katika dunia hii ya leo iliyo jaa social networks ambazo too much fake people pretending kuwa wema wakati all the need is publicity na kutengeneza hela kwa kupitia migongo ya wenye maisha duni na wenye upeo mdogo wa kupembua mambo. Ni ngumu kujua nani nikweli anania thabiti ya kusaidia au kuguswa na jambo la mtu na kufanya kile awezacho kusaidia hiyo hali bila kutegemea faida yoyote ile. Na hiyo ndiyo sababu mimi nampenda sana huyu dada yangu kwani siyo FAKE! Ni mtu wa kujishusha, anaongea na kupenda watu wote bila kujali “status” zao. Halafu sasa ana ile “free spirit” just like me ?? you know what I am talking about right?!  Yani Kama unataka ku have fun why kujibana bana? Go and have fun but accordingly to age appropriate! Siyo unakuta mama kalibia anaozesha bado anaangaika na show za kina “Yamoto bend” sasa teenagers nao wafanye nini?  FB_IMG_1451317288170Jamani naomba muelewe kwanini nawaongelea sana watu waaina hii ya Shy-Rose Bhanji zaidi. Unajua tuna wadogo zetu / wenetu  ambao wanatuangalia na kujifunza toka kwetu. Ambao wao napo itakapo fika muda wa kufunza kizazi kijacho watawafunza kile walicho jifunza toka kwetu? Sasa nini  tunawafunza? Au ni nini unataka wajifunze toka kwako?! Basi nafikiri sasa mtaniruhusu niendelee kupost habari au picha za dada yangu kipenzi bila shida. Kwani ameonyesha mfano mzuri katika jamii yetu na anastahili kuigwa na kupongezwa na watu wote! FB_IMG_1451317171897“Today, my Nieces and I spent our time with such wonderful kids (orphans) while donating food and other necessities to Mwandaliwa orphanage in Mbweni. I thank Allah for enabling me to be able to donate, spend time, give love and affection to the ones who are less fortunate. We complain about such little things everyday and aren’t grateful or appreciative of the little things we do have. It really breaks my heart because there are so many people out there who aren’t even able to eat today. We have to learn to appreciate the little things in life and give back every once in a while. I was very inspired with the kids and their caretaker… It’s a true blessing to be able to give back….Thank you Lord!” FB_IMG_1451325563312Hayo ni maneno ya wadada wa taifa letu ambayo yaliambatana na hizi picha hapo jana alipotembelea kituo cha watoto yatima huko Mbweni ambapo ndipo naye anaishi katika mji huo.

FB_IMG_1451317178369Najua hii haikuwa mara yake ya kwanza kufanya hivi. Ameshafanya hivi mara nyingi tuu. Ila kinacho mtofautisha yeye na wengine wengi ni kuwa huwa atafuti “wapambe” wakuongozana nao. Yani yeye hufanya kimya kimya tunakuja kuona picha tuu. Wengine ni lazima watangaze weee na kutafuta wapambe ndio waende. Yani hao wa hivyo ni kutafuta umaharufu zaidi kuliko nia dhabiti ya kusaidia. Na ndio maana kuficha tabia zao inakuwa ni ngumu kwani wakitoa huko bado wanarudi kutukana na kudharau hao hao maskini ambao walijifanya kuwapelekea misaada. Au utakuta ni ngumu sana kwao kujichanganya na masikini japo wana pretend to care about them. Ni waongo sana! Hivyo kwa hili la dada yetu siwezi sema hongera dada ShyRose Bhanji kwani hakufanya hivi ili kupongezwa na mtu bali for her own goodness! Sina sababu ya kumpongeza bali namuomba Mwenyezi Mungu mwenye wingi wa rehema na upendo azidi kumbariki huyu dada yetu kipenzi. Siwezi sema aendelee kwani hivyo ndiyo alivyo, bali azidi kumpa afya njema na uwezo wa kufanya haya mema ambayo anayafanya katika jamii yetu. FB_IMG_1451317198181Najua kuna baadhi ya watu watasema wapo wengi wanatoa misaada lakini hawajitangazi, we’ll nakubaliana na hilo! Naomba tuu ukumbuke ShyRose Bhanji hajajitangaza! Yeye alichofanya ni ku share picha kama anavyo share picha zingine za kumbukumbu ya vitu anavyo fanya hapa dunia as a good citizen of this world! Yani hii yeye ni tabia yake na si tukio la kutafuta umaharufu! Na naomba ujuwe kuwa hao wengine ambao wako kwenye level ya maisha au status ya dada yetu ShyRose Bhanji ambao hufanya vitu kama hivi bila kujitangaza au kuonyesha picha mitandao wengi wao huwa wana NGO zao na wanatumia hizo picha kupata hela kutoka kwa wafadhili nje ya inchi na ndio maana hawataki kuwa wazi kwani wanajua nia yao si ya kusaidia bali ni njia ya wao kupata kipato. Na ili watu wasijuie kile wanafanya basi wanaamua kufanya mamno kimya kimya! FB_IMG_1451325554663-1Jamani kwa mfano huu uliyo hai kabisaaaa hivi kunatatizo gani tukimfanya ShyRose Bhanji kuwa dada wa Taifa letu la Tanzania?! Kwani nani kanuna?! Mimi ndo nishasema hivyo ? Kuanzia leo hii ShyRose Bhanji ndiyo Dada Mkubwa wa taifa la Tanzania. Asanteni.  

Sister Sister!

FB_IMG_1451318456843-1Warembo hao. Vitukuu vya bibi yangu mkubwa. Pendeza sana. Nawatakieni siku kuu njema na  mbarikiwe wapendwa.

Kutoka Facebook

FB_IMG_1451318539789-1Pendeza sana Missy wetu (Former Miss Tanzania-UK) Hawa Gwao  Muke ya Boaz ?  FB_IMG_1451318510873Awii! Hicho kitanda kinaonekana kitamu sanaaaaaa mie hapo nikilala hata “mabox” naacha kubeba ?? upendeza sana. Nakutakia kheri ya mwaka mpya. Ubarikiwe sana na familia yako yote ?