HATA SAULI ALIKUJA KUITWA PAUL Injili ya Yesu kristu inaeleza kuwepo kwa Sauli aliyebadilika na kuitwa Paulo. Injili inamwelezea Sauli kama kiongozi wa kijeshi aliyekuwa ni katili kupita kiasi, asiyekuwa na huruma, aliye chukia, kuwatesa na kuwa hukumu kifo wana wa Mungu. Lakini pamoja na machukizo haya yote mbele za Mungu bado Mungu alikuwa na mpango mzuri naye.
Mpango wa Mungu ulikuja kutimia na Sauli akaitwa Paulo. Kupitia jina la Paulo, tabia zake zilibadilika na akawa mtumishi wa Mungu aliyeweza kuhubiri injili na kuandika vitabu vingi vya injili kuliko wanafunzi wote wa Yesu kristu alio wachagua na kuwapa kazi ya kueneza injili.
Hivyo sishangai kama Daudi akikimbia jina lake na kuitwa Poulo, maana yawezekana kwa jina la Daudi alikuwa mnyonge, kilaza, mvivu, mwoga, aliyefeli kwa kupata fa fa fa zote katika matokeo ya fom 4. Lakini kwa kuitwa Paulo emebadilika na kuwa jasiri, mchapa kazi, kiongozi mbunifu na mwenye kuthubutu, aliye faulu hadi chuo kikuu, aliyetenda makubwa katika uongozi wake kuliko hao wateule wa Mkuu.
#MyTake
Na Peter Sarungi (The next Speaker)
Kuna majina mengine yana Nuksi, hayaendani na ndoto zako na wala hayakusaidiiii. Unaweza ukawa una lalamika kushindwa kila jambo jema unalo jaribu kwa nguvu zote huku ukimshirikisha Mungu wako bila mafanikio kumbe ume sahahu kwamba jina lako halijabeba future unayotaka. Tuchunguze majina yetu hasa haya ya Ulaya.
Mwanangu Fidele siku akiona jina lake halimsaidii kufikia ndoto zake nitamruhusu na kumsaidia kubadili jina ???? Joks..
Niliwahi kusema kwamba vita alivyo chagua Makonda ni vita vinavyo hatarisha ustawi wa maisha yake. Mpaka sasa Mh. Makonda anapigana vita nne kwa yeye kuanzisha vita moja ya madawa.
1. Vita juu ya uhalali wa mali zake
2. Vita juu ya uhalali wa Elimu yake
3. Vita vya kisheria dhidi yake mahakamani
4. Vita dhidi ya Bunge na maazimio yake Maandiko matakatifu yanaeleza jinsi Yesu kristu alivyotoa kauli kwa wayahudi waliotaka kumwadhibu mwanamke aliye fumaniwa akizini kwa kutumia sheria za Musa……Alisema, “Kama kuna aliye msafi(asiye na dhambi) kati yenu basi na awe wa kwanza kumpiga mawe huyu mwanamke aliyefanya dhambi”
Hii ni kauli nzito sana kwa dunia ya sasa, Dunia inayotawaliwa na uwazi na kumbukumbu za kiteknologia, Dunia iliyo na macho pande zote, Dunia iliyojaa unafiki, usaliti, chuki, visasi, uongo, uzandiki, kashfa, fitina na machikizo mengi baina ya binadamu mmoja na mwingine.
Kwa Dunia kama hii… Ni vizuri tukaishi vizuri na jamii, tukaheshimu uongozi kam dhamana, tukajitakasa na dhambi kabla ya kuwatafuta na kuwahukumu wenye dhambi, tukajifunza kubakisha maneno ya kesho na keshokutwa.
Pole Mh. Makonda, ulianzisha vita moja lakini sasa unapigana vita nne tofauti.
Mungu akusaidie na akulindie roho yako isije ikapondeka kwa maneno na matendo ya binadamu wenzio…..Amina
Wema atinga Chadema bega kwa bega na mama yake! Limekuwa si jambo la kushangaza sana kuona mama Sepetu akiwa mguu kwa mguu katika maswala yanayo muhusu binti yake Wema Sepetu, japo kwa safari hii imekuwa tofauti kidogo na matukio mengine anayo yafanya!…….Wema amemwaga manyanga ya CCM na kubeba manyanga ya Chadema juu tena kwa madaha na mbwembwe nyingi huku mama yake mzazi akiziunga mkono na kuzibariki mbwembwe hizo!……. Je, nguvu ya mrembo huyo yatosha kumng’oa Magufuli / CCM madarakani?!! Mimi sijui kwani Siasa isn’t my cup of StrawberryMango smoothie! Bali naweza sema tuombeane uzima ili tushuhudie mambo 2020!……wishing her the best in her handover!
Ikatokea Mungu akakubariki kufika 2020 ukiwa hai na mwenye afya nzuri basi utakumbana na changamoto ya joto kali la siasa ambalo halijawahi kutokea nchini. Kwa Lowasa Edward, 2020 ni mwaka wake wa mwisho kujaribu kufikia ndoto zake za kutawala nchi, ni kama ana bunduki iliyobaki na risasi moja ndani ya mapambano, hivyo ni lazima apambane kwa akili sana tena kimya kimya ili kutafuta target sahihi ya kufyatua risasi yake kwa adui. Ndio maana kwa sasa Lowassa anajipanga kimya kimya akiamini matokeo yake ni 2020.Kwa JPM, 2020 ni mwaka wake wa kuimarisha utawala wake na hasa kupata matokeo yatakayo leta taswira ya kupwaya kwa upinzani nchini. Hivyo kwa sasa anajipanga kwa matendo na kwa mifumo ndani ya chama na nje. Kutokana na nguvu alizopewa Raisi kupitia katiba ya nchi, ni kazi nyepesi sana kutengeneza mfumo utakao kusapoti mbele ya safari hivyo tutegemee mifumo hiyo kukamilika 2019.
Kwa wananchi, 2020 ni mwaka wa majaribu sana kwao. Mpaka sasa bado wananchi wengi hawajui mwisho wa utawala huu ukoje, hawajui kama kutakuwa na mazuri ama mabaya ndani ya miaka hii mitatu iliyobaki (2017, 2018 na 2019) ikitokea uchumi wa mwananchi ukakua hadi kufika kipindi cha JK basi JPM atakuwa amepiga risasi ya ushindi kwa wananchi maana mpaka sasa amefaulu sehemu kubwa hasa ya ufisadi na nidhamu lakini amefeli kwenye UKATA wa wananchi, kuna malaika wameanza kuishi kama mashetani.
We would like to thank you for all the love and support you have given us over the course of our lives and for being in the midst of this exciting and memorable adventure. We appreciate each of you and recognize your participation. We’re honored that you came to celebrate and witnessed our love and vows to each other. To each and everyone of you, you mean so much to us and we’re beyond thankful to have you in our lives. Finally, to all of those who have given us their time and helping hands with planning this wedding, WE THANK YOU. From the bottom of our hearts we could not have done this without you.
Hardcore Truth! Huwezi kuoa au kutembea na warembo wote, wanawake wazuri siku zote wataendelea kuwepo, kila siku utakutana nao wapya. jifunze kuwa na adabu (self discpline) pamoja na kujidhibiti (self control).
Chagua mmoja tu, mjenge awe wako, mfanye awe malikia wako! hii itakupunguzia gharama, itakutunzia muda wako, drama pamoja na magonjwa.
Vile vile hakuna medali, tuzo au nishani ya juu ya ushindi wa kuwa na wanawake wengi, bali ni kuzifungia baraka ambazo Mungu anataka kukupa na kujipeleka mwenyewe kaburini mapema. Jiongeze brother!
Busara yangu; A realman sees no other females becoz he only has eyes for his girl! Mwl Tweve Hezron.
Hello wapendwa wasomaji wangu, natumaini wote hamjambo. Mie mzima wa afya hofu na mashaka ni nyie mlio mbali na upeo wa macho yangu 🙂 🙂 🙂 ……..wapendwa nime wamiss sana ila naomba mnivumilie tu simnajua nipo Bongoland na mambo ni mengi lakini soon tutarudi katika hali yetu ya kawaida na kwa nguvu mpya!…..Hata hivyo nawashukuru sana Halotel kwa internet ya uhakika! Nawasii wote tumieni mtandao wa Halotel kwa mawasiliano yenye viwango vya kimataifa!……..Nitarejea….!
Awwwih! Umesoma hiyo caption?! Isn’t that something! Nilisema last year around October or November kuwa Jokate is our “Princes Diana” she is going to be big kuliko unavyo fikiria and conquer the unconquerable! Keep on shining Jojo vijana wa Tanzania na Africa wanakutegemea sana. Show them the way! We love you!Wow! Mungu ajalie kheri tu kwani tunawakaribisha kwa mikono miwili!
Mr and Mrs Joseph Musira ndio Hottest And Best Couple of the Year!……Sababu haswa ya kuichagua hii couple kwanza nimeamua kwa mwaka huu ni enzi wazee wetu. Pili miaka 53 ya ndoa si kitu kidogo lazima kiheshimiwe! Napia ni kwasababu wanastahili!!……Basi ifuatayo ni historia yao fupi ambayo nitaieleza kwa kutumia picha zao za sherehe ya miaka 50 ya ndoa yao (Golden Jubilee of their wedding) ambayo ilifanyika huko Musoma, Mara miaka 3 iliyopita! Sherehe hiyo ilianzia kanisani ambapo walibariki ndoa yao na kuvaa pete ya nadhiri ya miaka hamsini!…….Haya furahia picha and Happy Valentine’s Day to you all! Maombi na kiapo yakiendelea ……….. Mr Joseph Musira na Felister Awiti wao ni wazaliwa wa mkoa wa Mara. Walikutana kwa katika kijiji kimoja kijulikanacho kama Kowak katika wilaya ya Rorya mkoani Mara. Felister yeye ni mzaliwa wa kijiji hicho cha Kowak akiwa ni mtoto wa kwanza wa mzee Cornel Awiti. Wakivishana pete baada ya ndoa kubarikiwa!…….Mzee Joseph Musira yeye ni Mwalimu kwa taaluma; hivyo wakati alipokutana na Felister alikuwa ni Mwalimu wa Kowak Middle School ambayo ipo chini ya missionary ya Wakatoliki. Kwasasa shule hiyo imebadilishwa na kuwa secondary ya wasichana ijulikanao kama Kowak Girls Secondary School ambayo mimi nilikuwa ni miongoni mwa wanafunzi walio fungua shule hiyo kwa mara ya kwanza. Mdogo wangu anaye nifuata kuzaliwa naye alisoma hapo! Picha ya pamoja na viongozi wa Diocese ya Musoma ambapo mzee Musira amekuwa mtumishi wao mpaka leo hii! Alianza kwa kufundisha kama Mwalimu, baadaye alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa shule zote za mkoa wa Mara ambazo zinamilikiwa na kanisa Katoliki mkoani humo! Ali stahafu akiwa katika cheo hicho zaidi ya miaka 5 iliyopita, lakini kwa uwadilifu wake na maadili mema kazini walimuomba kuongoza charity organization ambayo ipo chini la kanisa hilo hapo Mwembeni street, Musoma.
Cheti kiki kabidhiwa toka Vatican kwa Papa!….. Furaha iliyoje! Wakielekea ukumbini kwenye sherehe!…..Kama nilivyo waeleza hapo mwanzo kuwa Mzee Musira alikutana na bibi Felister katika kijiji cha Kowak akiwa Mwalimu. Basi naye bibi Felister alikuwa ni Registered Nurse katika hospitali ya Kowak Mission ambayo nayo ipo chini ya missionary ya Wakatoliki. Ambapo pia baba yake mzazi bibi Felister alikuwa akifanya kazi kama Clinical officer katika hospitali hiyo…….Miaka miwili baada ya wapenzi hawa kukutana waliamua kufunga ndoa, kula kiapo kitakatifu mbele za Mungu na uso wa dunia! Hapo ilikuwa tarehe 12 / September / 1964! Kama mnavyo jua kuwa maswala ya kuoa katika familia za Kiafrika si kitu cha mchezo kama wenzetu wa dunia ya Magharibi ambapo wapenzi wanaweza kuwataharifu wazazi wao kupitia Facebook, text msg, Tweeter, na Instagram kuwa wao wamepanga kuoana siku fulani na wazazi wakafurahia kabisa kwa furaha kuu! Hapana, ndoa ni agano takatifu lazima liheshiwe sana kwa kufata taratibu maalum za kimila na kidini! Basi ndivyo hivyo kama wafanyavyo wengine naye alifanya! Mzee Musira alifata mila za Waluo ili kuweza kumchumbia na kumuoa bibi Felister! Yeye aliambiwa atoe mahali ya ng’ombe 12 na pia amjengee mama nkwe nyumba ya mabati ya vyumba vitatu na sebule! Awwwh! Huu ukoo wa Awiti siyo watu wa sport sport ati 🙂 🙂 🙂 Si mnajua kuwa bibi Felister alikuwa msomi (Registered Nurse) wa nguvu 🙂 🙂 hivyo baba mtu hakutaka mchezo na binti yake! …….Ukisikia “mapenzi mubashara” basi haya ndo yenyewe kwani mzee Musira alitekeleza hayo masharti yote bila pingamizi! Hiyo nyumba ndio mama mkwe wake aliishi mpaka mauti ilipo mkuta mwaka 2014! Tutakiane mkono wa amani mpenzi wangu, tumetoka mbali sana. Asante sana kwa “mapenzi mubashara”…..,hayo yalikuwa maneno matamu kabisa kutoka kwa mzee Musira kwenda kwa la azizi wake bibi Felister ??? Champaign zikifunguliwa na watu wenye nyuso za furaha kabisa! Aliye vaa vazi la kitenge ni mdogo wake bibi Felister aitwaye Anna Cornel au Mrs Obure. Yeye ndiye anaye mfuatia Felister, ni Mwalimu mstahafu hapo Musoma. Baada ya kufunga ndoa bibi Felister ilibidi ahame kwenye nyumba aliyopewa kuishi kama nurse mkuu hapo mission na pia alibadili jina lake la mwisho kutoka Awiti kwenda Musira. Hapo ndipo walifanya maamuzi ya kuhamia Musoma, na miezi michache baadaye mzee Musira alipelekwa Germany kuongezea utaalamu zaidi katika fani yake! …….Waliishi Musoma kwa miaka kadhaa na baadaye mwaka wa 1970 waliamishiwa Moshi ambapo waliishi kwa zaidi ya miaka 10 kabla ya kurudishwa tena Musoma……. Mr na Mrs Musira wao wamebarikiwa kupata watoto 6. Watatu wa kiume (Musira, Gerald, na Peter) na watatu wakike (Eddina, Yasinter, na Neema). Eddina a.k.a Eddi yeye ndio mtoto wa kwanza na Neema ndio wa mwisho! Kwa bahati mbaya kijana wao aitwaye Peter yeye alisha lala usingizi wa mauti; hivyo hayupo nao tena! May his soul continue to rest in peace!Mungu pia amewajalia kupata wajukuu wanne! Wakiume watatu na wa kike mmoja! Wakinyweshana kinywaji maalum cha siku hiyo Mahaba mahabani! Kama walivyo shikamana siku ya kwanza pale Kowak basi ndivyo watakavyo shikana mikono yao mpaka mauti itakapo watenganisha! Waki kata keki kwa upendo na furaha Nilishe nikulishe ndio ishara ya upendo Mungu ni pendo. Penye Mungu kuna upendo mwingi na furaha isiyo elezeka! Hapa siongelei tu ndoa za “maigizo”, zile ndoa za ku-show off picha kwenye mitandao ya kijamii wakati ndani ya nyumba zenu wengine hawahemi! hapana! Naongelea real marriage, real commitment, honoring your vowels!!………. Miaka 53 ya ndoa hakuna michepuko wala mtoto wa “bandia”! Jamani, inawezekana!! These are real people in our communities; nina huwakika wapo wengine wengi tu!………Ee Mwenyezi Mungu endelea kumimina baraka zako kwenye hii ndoa na familia yao, Amen!
Katika wazazi ambao nawahurumia pia na mu-admire sana ni mama yake Wema Sepetu! Ni mmoja wa wazazi ambao wanapitia changamoto nyingi sana katika maisha ya kila siku kutokana na maisha ambayo binti yake ameamua kuishi; hivyo kahilo namuhurumia sana! Lakini kama nilivyowai kusema huko nyuma (somahapa) kuwa ni mama ambaye ananifurahisha sana na jinsi anavyo simama bega kwa bega na binti yake, katika mabaya na mazuri! Kwa wazazi wa Kiafrika ni ngumu sana! Wachache mno wanaweza fanya afanyavyo mama Sepetu! Na kwasababu hiyo anakua mfano mzuri sana wa kuigwa! Mtoto wako ni mzigo wako mpaka kifo. Huwezi mkana au mkataa mtoto wako eti kwasababu tu haendani na maisha utakayo! Big up mama Wema!
Na Peter Sarungi (Next Speaker)“Vita ya dawa za kulevya haina umaarufu, haijalishi ni mtoto wa nani anahusika, hata kama ni mke wangu anahusika mkamateni” Raisi Dkt. Magufuli…….Katika vita hii, nilikuwa nasubiri kauli ya mkuu wa kaya ya kutoa support ya ulinzi, usalama na hata kubariki vita hivi alivyo vianzisha Mh. Makonda (RC. Dar) Kauli alizozitoa Mkuu wa kaya wakati wa kumwapisha Mkuu wa Majeshi Tanzania yana ashiria ushiriki wa moja kwa moja wa mkuu wa kaya. Majibu ya JPM kwa kauli ya Mh. Nape ni firimbi kwa viongozi wengine wanao leta sababu nyingi za kunyamazisha vita hii wakati vijana wana angamia.
“Kauli ya Raisi ni agizo linalo hutaji utekelezaji bila kusita” Peter Sarungi @2017