




















Wakulia amefurahia kumuona babu wakati wa kushoto amefurahia kumuona baba mkubwa! Ukitaka watoto zako wapende ndugu zako lazima uwafundishe muhimu wa ndugu zako kwako wakati wakiwa bado wadogo. Nasio kuwafundisha kwa maneno bali kwa vitendo. Siku zote watoto watasikia unachosema LAKINI watafanya kile ambacho wanaona mzazi unafanya. Wewe ndio ubao wao wakujifunza na watakusoma vizuri sana, basi hakikisha unacho andika kwenye ubao wako nikile ambocho kweli unataka watoto wako wajifunze toka kwako.

#ToGodBeTheGlor

Kuna binadamu wenye tabia za kama huyu Nyani anaye mvuta mwenzie mkia. Yani mtu anatumia nguvu za ziada kutaka kumuangusha fulani kwasababu tu anamzidi mahala fulani.
Ukweli usiopingika ni kwamba nguvu anyopoteza kumvuta mwenzake chini ni kubwa sana kuliko nguvu ambayo angetumia kufikiria apandaje juu ya mti! Kama angeweza kujitathimini na kujua wapi anakosea halafu angeamua kutumia nguvu hiyo hiyo kupanda juu nafikiri huwenda angekuwa mbali zaidi ya huyo anaye mvuta chini.
Hivi ndivyo baadhi ya watu walivyo. Wanachukua nguvu nyingi kimchukia mtu au watu ambao hawana uhusiano wowote katika kushindwa kwao au kutokufanikiwa kwao. Badala ya kujitathimini wao wanajenga chuki. Kwamfano, embu fikiria kama huyu Nyani anaye mvuta mwenzake kama angeamua kuzunguka upande wa pili wa mti akatumia hiyo nguvu kupanda unafikiri angekuwa wapi? Huwenda angekuwa amefika juu ya mti akapunga na upepo mwanana huku akimchora mwenzie!
#TafakariJuuYaMaishaYako #AchaChukiHaijengi
Siku zote hakikisha unavaa viatu vinavyo kutosha! Usivae viatu vikubwa kuliko miguu yako ili nawe upendeke na wenye miguu mikubwa! Na usivae viatu vidogo kuliko miguu yako ili tu ufurahushe wenye miguu midogo! Na kamwe, usitembee bila viatu ili tu ukubalike na wanao penda kutembea peku peku!
Maisha ni mafupi sana lakini safari yake ni ndefu ambayo barabara yake haijulikani wapi kuna lami na wapi kuna vumbi (rough road) hivyo ni vyema kuvaa viatu vinavyo kutosha wewe mwenyewe siyo ndugu yako wala rafiki kwani wewe mwenyewe ndio utakaye tembea hiyo safari ya maisha yako. Bahati mbaya kila mtu kupangiwa bara bara yake na kila bara bara inachangamoto zake huwezi azima viatu ambavyo hujui kama vitamudu safari yako!
Hivyo, ili ufurahie safari yako kwanza, hepuka kuiga miondoko ya watu wengine. Wewe unaweza fikiria fulani anatembea kwa madaha ngoja niige miondoko yake kumbe mwenzako anamaumivu ya miguu kutoka bara bara yake. Pili vaa viatu vya size yako visiwe vikubwa wala vidogo, na kama huwezi tembelea viatu virefu basi vaa viatu vya chini au boots! Mwisho, ukichoka unaruhusiwa kupumzika ila usilale bara barani hakikisha unapigania kufika mwisho wa safari.