Chuki, ubaguzi, na upendo mtoto ufundishwa na wazazi wake!

Chuki na ubaguzi mtoto ufunzwa na wazazi wake kama ilivyo upendo! Mtoto anazaliwa na kichwa che ubongo mtupu na safi! Sasa wazazi na walezi wa hawa watoto ndio inategemea watajaza huo ubongo wa huyo mtoto na vitu gani! ........Nisawa na elimu kuhusu Mungu, mtoto hawezi jua umuhimu wa kuabudu na kumcha Mungu kama wazazi na walezi wake hawakumfundisha na kumuonyesha kwa vitendo kuwa kuna Mungu anaye stahili kuheshimiwa na kuabudiwa! Au utakuta Mzazi anamwambia mtoto wake hiyo nguo mbaya mpe fulani (ana taja jina la mtoto mwingine) hivyo mtoto anakua akijua kuwa kama kitu kibaya au kimezeeka ndio unagawa kwa wengine! Ambapo ni makosa makubwa sana! Mzazi mfunze mtoto wako kupenda watu wote wa rangi zote bila kujali kipato chao cha kiuchumi!

Tamera amenifanya nijisikie kuolewa na mzungu ??? I’m curious to see how my baby will look like ??

Leave a Reply