Familia katika kusaidiana….!

 Ukweli hata kama familia mnapendana kiasi gani lakini kama hamshirikiani katika maswala ya kujiinua kiuchumi, kiroho, au katika maendeleo yoyote yale basi upendo wenu ni BATILI! Yani ni upendo wa "kichina" 
    Sijasema kuwa familia itakuwa haijakamilika (perfect) hapana! Hapa duniani hakuna familia ambayo imekamilika! Kila familia ina matatizo yake, jinsi mnavyo kabiliana kutatua hayo matatizo ndio inawafanya mjulikane nyie ni familia ya watu gani. Njia mtakayo tumia kutatua matatizo yenu inawezekana iwe njia ambayo wengine wataona ni sahihi au sio sahihi lakini kama kuna upendo wa kweli basi hayo yatabaki kuwa maoni yao kwani kwenu nyinyi wahusika kila kitu kitaonekana sahihi! 

Pichani ni familia ya mzee O.O Igogo katika moja ya business dinner iliyofanyika jana Dar, Tz

Leave a Reply