#FBF #Mahojiano na Linda Bezuidenhount

11249848_709423412497306_3810608941086466482_nFB_IMG_1472436063790Leo nimeamua ku “Flash Back” videos za interview ambazo nilifanya na mwanamitindo wa kimataifa Ms. Linda Bezuidenhout mnamo mwezi wa Pili mwaka jana 2015!

Hapo juu ?nisehemu ya kwanza ya mahojiano. Na hapa chini ? nisehemu ya pili au ya mwisho ya mahojiano yetu.

FB_IMG_1472436063790Haya yalikuwa ni mahojiano yangu ya kwanza kabisa kufanya huku nikirekodiwa. Nilipewa hii nafasi ghafla, yani nilijua nataka kufanya mahojiano na Linda lakini sikujua lini yatafanyika. Mara ilikuwa siku ya juma Tatu napigiwa simu na kaka yangu Dj Luke wa Vijimambo blog nakuambiwa kuwa Linda ametukaribisha kwake siku ya Juma Mosi na yupo teyari kufanya mahojiano nami! Nilisita, lakini kaka yangu akasema nitaweza nisiogope! Basi hivyo ndivyo ilivyokuwa. Kama hujawahi yaona basi nakuomba uyatazame na niruhusa kutoa maoni yako! ……….Kwakweli siku zote nitamshukuru sana Linda kwa nafasi hii aliyonipa na pia sito choka kuwashukuru kaka yangu Dj Luke wa Vijimambo blog pamoja na mtani wangu Mubelwa Bandio wa Kwanza Production kwa kunisaidia kufanikisha hii ndoto. Sina chakuwalipa bali nawaombea baraka siku zote! ??

Leave a Reply