Happy New Year my beloved!

Happy New Year to my good readers! Binafsi namshukuru sana Mungu kwa kuweza kunipa nafasi nyingine yakufanya matengenezo katika maisha yangu kimwili na kiroho, kijamii na kiuchumi! Jina lake litukuzwe siku zote!

Mwaka niliufunga kwa kuanzia kanisani kuabudu siku ya Sabato kisha tukaenda na mdogo wangu kula mihogo Coco beach! Baada ya hapo mida ya jioni nilikwenda msalimia baba yangu mkubwa Charles O. Igogo na familia yake wao wanaishi hapo OysterBay. Tulikaa hapo mpaka majira ya saa nne usiku kisha tukarejea nyumbani. Tukapiga story na kufurahi pamoja!…… Siku ya tarehe moja 2017 ndio tulihama rasmi ambapo palikuwa makazi yetu ya kudumu kwa muda wa zaidi ya miaka 30! Hivyo sasa naweza sema rasmi kuwa tumehama Keko Juu na sasa tunaishi Kibada, Kigamboni!

Sarah (left) na Magreth

Basi siku ikaisha kwa kwenda kwenye mgahawa mmoja hapo Kibada ujulikanao kama Silver Shark tukiwa mimi, baba yetu, mdogo wangu Magreth, na my niece Sarah. Tulikula Mbuzi, kuku, na chips za kumwaga! Sorry picha zote zilipigwa na simu ya baba amesafiri kabla sijazitoa ?? Tunamshukuru Mungu kwa yote!…….Too bad sitaweka ahadi yoyote ile kwa blog kwani I’m a woman and certainly I’m allowed to change my mind  🙂 🙂 🙂 Happy New Year Everybody!Be blessed! ? ??

Leave a Reply