alphaigogo.com
Hongera sana Cecilia - alphaigogo.com
Hongera sanaaaaaa binti yetu Cecy kwa kumalizia elimu yako ya msingi. Huu uwe ni mwanzo tuu, tunakuombea uwendelee mpaka upate ile elimu ya juu ambayo Mungu ataona inakufaa kupata. Mungu akutangulie, akakushindie majaribu yote na ukaishike sana elimu usiiache. Hongera sana dada yangu na shemeji yangu kwa kukuza binti. Mungu abariki uzao wenu wote. Kwa mara nyingine tena, hongera sana Cecilia.
Alpha Igogo