Je, unaheshimu mali za watu?!

Alpha Igogo, blogger Throw ? 2008

Mimi naheshimu sana kitu cha mtu yoyote yule! Yani mtu akiniazima kitu au kunipa kitu huwa nakitunza zaidi ya chakwangu! Naonaga mpaka mtu kutoa kitu chake kakupa au kukuazima inamaana sio tu amekuheshimu bali anakuamini! Trust is essential to me! Nina picha nilipewa na wanafunzi wenzangu Kowak Girls secondary school hizo picha mpaka leo ninazo hapa Marekani, sidhani hata kama wao wanakumbuka! Hivyo ndivyo nilivyo mimi! Na huwa nachukizwa sana nikiona mtu haeshimu kitu cha mtu mwingine kwani inaonyesha wewe unaweza kuwa na vielement vya tabia za kichawi chawi ???

Sasa jana jioni nilikuwa natafuta kitu kwenye closet (ambapo kuna washer and dryer sio kwenye nguo) nikakutana na hii GPS! Yes that how GPS monitors used to be ?? Wahenga mtatujua tu! ? ?Hii GPS niliazima kutoka kwa my good friend aitwae Sammy mwaka 2009. Alikuwa akihiitaji nampelekea nami ikitokea nahitaji naifata au ananiletea. Mwishowe ikaishia kwangu. Kusahau na mambo kuwa mengi sikufanikiwa kumrudishia.

Lakini kwakuwa nilijua niliazima sikupewa moja kwa moja miaka yote nimejisikia kuwa na wajibu wa kuitunza mpaka hapo nitakapo mpa tena. Believe me, nilipokuwa nahama Michigan to Texas, niliipaki vizuri nikaja nayo ?? nimeihifadhi vizuri sana mpaka stand yake ipo ? nafikiri it’s about time kumrudishia mwenye GPS yake akitaka kuitupa aitupe mwenyewe! Sindioo au niendelee kumtunzia kama yeye alivyokua akinitunzia vya kwangu ???? #HeshimuVyawatuZaidiYaChako

#NiMchezoWakutunzianaTu

 

 

Leave a Reply