Jokate Mwegelo: Kitu cha kwanza awe na hofu ya Mungu!

Wow! Nimefurahije!! Nilikwenda kwa YouTube kutafuta video fulani ya Jokate (zile za kuwa mgeni rasmi shule ya Mugabe, please Jojo ziweke kwa YouTube) nikakutana hii short interview kati ya MCL Extra na Jokate. Ni interview fupi lakini nimeipendaje sasa!! Jokate anasema anatamani sana kuwa na familia and she can't wait for it to happen! Na kuwa mwanaume anaye mpenda kitu cha kwanza lazima awe na hofu ya Mungu! ......... Well, kwanza pole sana Jokate kwa kuuguliwa na baba, mkono wa Mungu wa uponyaji uwe naye, na amani ya Bwana iwazunguke wote. Pili, Safi kabisa kumtaka mwanaume ambaye ana hofu ya Mungu siyo tu ya mdomoni bali kwa matendo yake! Mwanaume ambaye atakuwa teyari kwa hiyari yake kusema tupige magoti tuombe! Siyo wewe ndio umlazimishe kusali. Unataka mwanaume ambaye mkipata shida atasema tumkimbilie Mungu siyo waganga wa kienyeji na dini za mazingaombwe! Kama mapenzi ya Mungu basi akupe mwanaume mwenye imani sawa na wewe! Sikatai wapo watu walio owana wa imani tofauti lakini lazima tukubali kuwa hakuna kitu kigumu kama kulea watoto katika imani mbili tofauti!! Pia ukiomba mwambie Mungu akupe mwanaume ambaye hayupo kwenye spotlight sana kama wewe (Yani asiwe mtu wa kutafuta followers na likes kwenye social media) someone in a corporate world siyo siasa wala entertainment industry! Someone with strong family values kama wewe. Anayependa na kujali ndugu zake kwani huyo atakuwa anaelewa nini maana ya familia. Ukiona mwanaume kaowa au kafanikiwa kidogo tu halafu ndugu zake kawabwaga muogope kama ukoma! Something must be seriously wrong somewhere! Na huyo mwanaume awe mkarimu and fun to be around, Nani anataka mwanaume mwenye gubu?! Au kutwa kuvimbisha masharubu kama chura ?? ..... I strongly believe Mungu atakupa very soon! You're such a phenomenal young lady with a bright future! Tena akubariki uzao wako wa kwanza uwe mapacha wa kike na kiume ????? babysitter nipo ??

Leave a Reply