Jumbo Camera House ni duka bora kwa mahitaji yako ya Camera za aina zote!

Jumbo Camera House ni moja ya sehemu ambayo nilikwenda nikiwa Tanzania nikapata customer service nzuri sanaaaaaa! Camera yangu ilikuwa inanisumbua kwenye setting na battery  ilikuwa inaisha kwa muda mfupi hivyo nilihitaji wataalamu kuniangalizia tatizo ni nini na pia wanifanyie setting. Kwakweli hawa watu walitufanyia mapokezi mazuri sana japo Camera hatukununua kwako (ilikuwa ni zawadi) hawakutuonyesha “nyodo” za aina yoyote ile! Walikuwa very professional, friendly and welcoming! Tulihudumiwa vizuri sana and Yes! I bought something kuwaunga mkono as all the services walitufanyia ya kuangalia tatizo kwenye battery na ku-program my camera  walisema hatuhitaji kulipa was just free!…….Jamani msifikirie hawa hawatu walikuwa wanatujua hapa!! Hawanijui, na hata mimi na mdogo wangu tulikuwa hatuwajui tulienda kwao as to see kama wataweza kutusaidia, hivyo naamini kama walituhudumia sisi kwa furaha na upendo namna hile basi inanifanya niamini kuwa hivyo ndivyo walivyo kwa wateja wao wote!Hapo ? ni address yao na njia zao za mawasiliano kama utahitaji kupata huduma zao!

Leave a Reply