Kesha la asubuhi: Kufukuza giza

                *KESHA LA ASUBUHI*              

                         JUMATANO

                          23/05/2018

                 *_KUFUKUZA GIZA_*
?_Ondoka, uangaze; kwa kuwa nuru yako imekuja, Na utukufu wa Bwana umekuzukia. Maana, tazama, giza litaifunika dunia, Na giza kuu litazifunika kabila za watu; Bali Bwana atakuzukia wewe, Na utukufu wake utaonekana juu yako. Isaya 60:1, 2._

✍?Kanisa limeteuliwa kuwa njia ambayo kupitia hiyo nuru takatifu inapaswa kuangaza katika giza la kimaadili la ulimwengu huu, na miale yenye kuleta amani ya Jua la haki kuanguka juu ya mioyo ya wanadamu. 

✍?Kazi ya binafsi kwa mtu mmoja mmoja na kwa familia hufanya sehemu ya kazi ambayo inabidi ifanywe katika shamba la Bwana la mizabibu ya kimaadili. Upole, ustahimilivu, uvumilivu, upendo wa Kristo ni lazima vidhihirishwe katika kaya za dunia. 

✍?Kanisa lazima liinuke na kuangaza. Wakiwa angavu kwa Roho na nguvu ya ukweli, watu wa Mungu ni lazima waondoke na kwenda katika ulimwengu unaolala katika giza, ili kudhihirisha nuru ya utukufu wa Mungu. Mungu ametoa kwa watu uwezo bora wa akili ili utumike kwa ajili ya heshima yake, na katika kazi ya umisionari nguvu hizi za akili zinaitwa katika utendaji hai. Uboreshaji na ukuzaji wa hekima wa karama hizi za Mungu utaonekana ndani ya watumishi wake. Siku kwa siku kutakuwapo na ukuaji katika kumfahamu Kristo.

✍?Yeye aliyewahi kusema kwa jinsi ambavyo kamwe hakuna mwanadamu aliwahi kusema, aliyevaa vazi la ubinadamu, bado ni Mwalimu Mkuu. Kadiri unavyofuata katika nyayo zake, ukiwatafuta waliopotea, malaika watasogea karibu, na kupitia katika nuru ya Roho wa Mungu, ufahamu mkuu zaidi utapatikana kuhusu njia na mbinu bora za kufanikisha kazi iliyowekwa mikononi mwako. …

??‍♂```Wale ambao wangelikuwa nuru ya ulimwengu wameangaza miale dhaifu na milegevu tu. Nuru ni nini? Nuru ni uchaji Mungu, wema, ukweli, rehema, upendo; ni udhihirishaji wa ukweli katika tabia na katika maisha.

??‍♂ Injili inategemea uchaji Mungu wa waumini wake binafsi kwa ajili ya nguvu zake za kuleta maendeleo, na Mungu ametoa kinachotakiwa kupitia katika kifo cha Mwana wake mpendwa, ili kwamba kila roho iwezeshwe kikamilifu kutenda kila tendo jema. Kila roho inapaswa kuwa nuru kali inayong’aa, ikionesha sifa zake yeye aliyetuita kutoka katika gizani na kuingia katika nuru yake ya ajabu. -Review and Herald, March 24, 1891.```

*MUNGU AWE NANYI MNAPOJISOGEZA KARIBU NAE. AWABARIKI WOTE*

Leave a Reply