Kheri ya kutimiza miaka 8 ya ndoa yenu!

 Kheri ya kutimiza miaka nane ya ndoa yenu Mr and Mrs Rweikiza! Nawatakieni furaha na amani tele katika maisha yenu na upendo mwingi ndani ya familia yenu na watu wote wanao wazunguka. Happy belated Wedding Anniversary  (06/20)!.. .... Mbarikiwe sana.

Btw, naomba leo kwa mara nyingine nimshukuru sana mtani wangu  (Mr. Rweikiza) for a kind act that he did to me way back then in Wichita! Sema this time nitasema hapa kwa blog! Napenda kukushukuru sana kwa ukarimu wako uliyonifanyia wakunipeleka kufanya Road Driving Test ili nipate Leseni ya kuendesha gari hapa Marekani! Ubarikiwe sanaaaaaa na familia yako!  Haya ngoja niwape story ilivyokuwa; mara ya kwanza nilipelekwa na my brother Mwiga Kapya (where is he?) lakini sikupita mtihani, yule mtu aliyenifanyia road test alisema sikufanya "completely stop"  kwenye stop sign ?? hivyo hakunipa! Sasa ikabidi nipange siku nyingine, nafikiri ilikuwa baada ya wiki hivi! My brother Mwiga akawa amebanwa na ratiba hivyo akamuomba Mr. Rweikiza anipeleke!Kuja kumbe alikuwa ni mtani wangu! Wahaya oyeeeeeeeee! Lol! Sijui ni kwanini lakini nimejikuta most of my sincere, kind friends ni Wahaya! I think I will never get away from them  ?? Mtani wangu, asante sana. And Happy 8th Anniversary!

One thought on “Kheri ya kutimiza miaka 8 ya ndoa yenu!”

Leave a Reply