Msikilize Aunty Ezekiel akieleza historia yake na Moses

 Kama kuna wapendanao ambao nawapenda sana kwenye hii kitu inaitwa Bongo movie / Bongo flava basi ni hii couple! Mie sijawahi kaa kuangalia Bongo movie toka enzi ya Mambo Hayo (wahenga mtatujua tu ?) hata movies za marehemu Kanumba sijawahi kaa nikaangalia!Mimi siogopi kusema ukweli as truth will always set me free napia inanipunguzia marafiki wasio na tija ?? Mambo ya hawa wasanii wa siku hizi honestly yana nikera sana! Wengi tunawajua kwa scandle zao kuliko talent zao! Lakini kwakweli lazima nikubali kuwa Aunty na Moses wamenifanya nianze kuwachambua mmoja mmoja nakugundua kuwa kumbe kuna wengine wanajielewa na huwenda ipo siku moja nitakaa chini kuangalia Bongo movie tena! Natamani wasanii wakike wa aina zote wangekataa huu udhalilishaji wa wanawake unaotumiwa na promoters na media eti "kutafuta Kiki" kwa kuwekwa kwenye scandle zisizo na kichwa wala miguu ili kazi yako au kipaji chako kionekane! Huu ni udhalilishaji period!! Kama mtu ana talent tafuta njia sahihi ya watu kuona talent yake nasio kuwapa kashfa za kutembea na wanaume!! If someone got talent people will see it!! Chema chajiuza kibaya chajitembeza!!!

Anyway, back to Aunty Ezekiel na Moses wake, kumbe jina la Aunty ni jina lake halisi aliyopewa na baba yake! Mimi nilifikiria ni jina la kuigiza ? ......Halafu wewe Moses wewe huyo shetani aliyekuingia sijui alitokea wapi, sasa sisi tungemuona wapi Cookie?! ......... Please people interview ipo very raw  yani Aunty Ezekiel kafunguka haswa lakini usishangae sana kwani hayo ya kutoa mimba na kwenda kwa waganga ni mambo alifanya wakati huo yupo kwenye "giza nene" Ni mambo ya kale! Don't judge  if you know what I mean ???  Hey every Saint has a past, every sinner has a future, and who are you to judge anyone!

Leave a Reply