Mzaha, mzaha, hutumbua usaha!

Katika maisha kuna vitu vya kufanyia mzaha na vingine usijaribu hata siku moja! Kitu chochote kinacho husisha HISIA za mtu usifanyie mzaha hata siku moja! Kumbuka hisia za mtu ndizo zinazomfanya huyo mtu kuwa mtu, sasa kuzichezea hisia za mtu kwanza ni unyanyasaji wa hali ya juu, pili unaweza kuleta madhara makubwa sana kwa muhusika ambayo saa nyingine yanaweza sababisha kifo! Siku zote kumbuka  "mzaha, mzaha utumbua usaha"! Naomba niongee na watoto wa kike kwa hili, ogopa sana mwanaume anayekufanyia vituko halafu badala ya kukuomba msamaha anakimbilia kwa ndugu na marafiki zako kujisafisha kuwa alikuwa anatania tu au kukufanya wewe uonekani ni mtu ambaye ni tabu to get along with! Kama hujaoana na huyo mtu basi kaa naye mbali kabisa kwani huyo mtu ni MNYANYASAJI! Na anachokifanya hapo ni kuweka mazingira mazuri ya kukunyanyasa pindi atakapo kuoa na wewe usiwe na pakukimbilia kwani amesha "brainwashed" watu wako wakaribu kuwa wewe ni hard personal to get along with au wewe ni mtu unayechukulia kila kitu too seriously!! 

Mtu anayecheza na  hisia zako bila ya huruma huyo mtu ni wakuogopa kwani hisia za mtu siyo jambo la kuchezea! Halafu unapo taka kuliongelea wewe ndio mtu mbaya?! Kwa mfano, eti mtu anakudhalilisha kwa kupiga picha na mwanamke aliye zaa naye au mwanamke aliyekuwa akimdeti kabla yako nakuweka hizo picha kila kona za media halafu anasema "was just a joke"?! Tena anafanya hivyo zaidi ya mara moja? My friend, mkimbie huyo mwanaume kama unavyoweza kukimbia kifo! Unless unataka kuwa "celebrity" basi utakubaliana na unyanyasaji huo simnamuona Zari anavyo fanyiwa na Diamond?? Ndo Ucelebrity huo 🤣🤣🤣 No! Ain't Zari! I'm just a normal girl from KekoJuu who deserves love, respect, and happiness 😍😍  Au kwa mfano, mlisikia ile mvua kubwa iliyonyesha hapo Dar es salaam  ambayo ikasababisha maafa makubwa sana na watu kupoteza maisha? Sasa wewe ndio mwanamke unaishi Dar es salaam, maeneo ya Jangwani, halafu mwanaume yupo Morogoro cha ajabu hata kukupigia simu kujua kama upo salama au umekufa hakuna! Tena unamuona yupo online akifanya yake? Then mtu huyu akisema anakupenda wewe  mtoto wa kike bado unamuamini?!! 🤔🤔🤔 Unless you want to marry your killer ndio utakubaliana na huo upuuzi kwani wanaume wa hivyo hakuheshimu wewe wala mahusiano yenu! Mwanaume wa hivyo hakujali wewe wala roho yako! Yani kifo chako hakimsumbui! 

Ukiyakubali mambo kama hayo kabla hujaolewa halafu ukaja olewa na huyo mtu basi tegemea hizo tabia ataendelea nazo mpaka ndani ya ndoa yenu na hautakuwa nalakusema! Atakapo sema mbona hayo nilikufanyia kabla ya ndoa na ukakubali kunioa utasema nini?! Au mfano mwingine, mwanaume anataka kukuoa wewe lakini mipango ya maisha yenu anaongea na watu wengine bila kukuhusisha?! 🤔🤔 What does that tell you? You are just going to be a "trophy wife"!! definitely that is not a man to have family with!! Ipo siku atataka kukutoa roho yako halafu atasema alikua anataka kuona how will you react!! Emotional abuse siyo kitu cha kufanyia mzaha hata kidogo kwani mzaha, mzaha hutumbua usaha!

Leave a Reply