Ruge Mutahaba: lazima tufanye kitu kikubwa kwa ajili ya historia ya nchi hii

@Regranned from @cloudsfmtz - Hatujahitimisha bado huu ndiyo mwanzo hatuwezi kuishia hapa tukaliacha kama Tamko sisi kama CMG tutalibeba kama Azimio kufika mwisho. Tumezunguka zaidi ya miaka 5 tumesikia vilio vinavyofanana kwa Vijana kabla hatujakwenda mbele lazima tufanye kitu kikubwa kwa ajili ya historia ya nchi hii. Jana tumeanza kwa kujiuliza Kwa swali Je tunaimba wimbo mmoja kwa Sauti zenye kufanana? Inawezekana hadi tunaondoka hapa bado hatujapa Sauti moja Lakini naimani tutafikia lengo. Tunaposema anzia sokoni lazima tuangalie Uongozi wa kimasoko namna gani tunaweza kushindana pasipo kushushana kwenye mazingira ya ushindani, Ubakie kwenye maneno tu na Vitendo vionekane Sokoni.  Hebu tujaribu kutafuta taarifa na lazima wote tukubaliane kusaidia na maafisa kilimo na viongozi katika kuodoka katika Kilimo cha Kisasa. Sababu kilimo chetu kimepitwa na wakati. Kama tuna uwezo wa kupata mifumo bora zaidi katika huduma za kijamii tujipe Moyo na wala tusivutane kama kuna Fursa zipo tuzikimbilie katika kuzalisha huduma bora zaidi. Misingi yetu lazima ijikite katika namna ya kusolve tatizo bila kulalamika, Malalamishi tunayoishi nayo yageuke kuwa changamoto ambazo ni fursa kwetu tutengeneze kitu kinachoitwa Problem Solving Skills. Ndani ya Mwezi mmoja unaofuata kuanzia sasa kupitia WAMANTA waliopo hapa, Watu wa kwenye mitandao pamoja na wengine walio pamoja nasi tutatengeneza timu kwa ajili ya andiko la Azimio la Kagera. kabla ya Bunge la bajeti 2017/18. Hili #AzimioLaKagera Leo kwa pamoja tumeandika historia kubwa sana namshukuru mwenyezi Mungu kupata viongozi wa dini ambao tumeshindana nao kuanzia siku ya Jana hadi leo ni faraja kwetu. Kwasisi tuliobahatika kuishi leo lazima tubadilishe mtazamo wa kuitengeneza Kagera mpya yenye mtazamo mpya kama mipaka ya kiuchumi na siyo eneo la Ulinzi wa mipaka yetu.

 Muasisi wa Fursa
 Ruge Mutahaba.
 #AzimioLaKagera @tatumzuka - #regrann

Leave a Reply