Sasa angevaa kimini si ingekuwa ugomvi?-M.M Mwanakijiji

Screenshot_2016-06-28-14-14-16-1Neno la Kejeli:  Sasa jamani, hata kama ndio kujiita “wakosoaji” ndio imekuwa kukosoa hata Naibu Spika kwa vile kavaa suruali na anaosha magari? Sasa angevaa kimini si ingekuwa ugomvi? Halafu, wenzetu hawa mkienda kwenye nchi za watu huwa mnatembea mmefumba macho? Mbona mnaweza kupata shida maana unaweza ukadhani kila mtu kajidhalilisha kwa nguo alizovaa. Ukweli ni kuwa Naibu Spika katoka vizuri, kapendeza, na katoka kwa heshima.

2016-06-30 09.17.03Akili za watu wengine zimejaa ushetani! Saa zote mambo yao na maongezi yao ni kuangalia vitu au watu katika mtazamo hasi! Tabia ya mtu haipimwi au haiangaliwi kwa kutumia mavazi mtu anavaa, kama ni hivyo basi wanawake wa Al-Qaeda wangekuwa Malaika! Lakini nguo wanazo vaa na mambo wanayotenda ni tofauti kabisa!…………Kuna wanaume ambao akili zao zimejaa uchafu wa ngono tu! Na hii haijalishi mwanamke amevaa vipi bali ni wao wenyewe na akili zao. Na hawa ndo wanaume unakuta wanabaka watoto wadogo. Sasa mtoto naye alivaa nguo fupi? Ni akili zao na uchizi wao!FB_IMG_1467295641922

Leave a Reply