Sherehe ya maisha ya mwisho ya mama Yucabeth Atieno Chaulo!

Marehemu Mama Yucabeth Atieno Chaulo enzi ya uhai wake!

Siku ya Alhamisi ya tarehe 24, mwezi wa Sita, mwaka huu (06/24th/2021) familia ya marehemu mzee Androniko Chaulo walipatwa na msiba wa mama yetu Yucabeth Atieno Chaulo, kilichotokea mida saa mbili usiku huko Dar es salaam, Tanzania. Na amezikwa leo kwenye makaburi ya ukoo wa Chaulo yaliopo katika kijiji cha Buturi, wilaya ya Rorya mkoa wa Mara, ambako ndipo makazi ya kudumu ya ukoo wa Chaulo.

Pichani juu ni mama yangu mzazi (mwenye Tie dye) pamoja na marehemu. Mapema mwaka huu alipokwenda kutembelea makazi ya mama yangu huko Kibada, Dar es salaam.

Mama Yucabeth Atieno Chaulo ni mama mzazi wa Shemeji yangu mkubwa Mussa Chaulo a.k.a baba Danny. Shemeji Mussa amemuoa dada yangu mkubwa Elline Igogo a.k.a mama Danny takriban miaka 21 na miezi kadhaa sasa. Wamebahatika kupata watoto watatu Daniel, Chaulo, na Cecilia.

family!

Akiwa na baadhi ya watoto zake, wakwe zake, mama yangu mzazi, na mdogo wangu (mwenye darkblue), Kibada Dar es salaam.

Bahati mbaya miezi kama mitatu hivi iliyopita marehemu mama Yucabeth Atieno Chaulo alimzika mmoja wa binti zake ambaye yupo kwenye picha hii, (wapili kutoka kushoto mwa dada mwenye nguo Nyekundu, nyuma ya mama yangu naye amevaa Tie Dye)! ….. Roho zao zipumzike kwa amani ya Bwana.

Mama yetu alikua akisumbuliwa na mapafu kwa muda mrefu kidogo, alikuja Dar es salaam kwaajili ya matibabu na ndipo mauti ilipomkutia. Kwa asili yeye ni Mkenya (mzaliwa wa Kenya / mluo toka Kenya) ambaye aliolewa ujaluoni huko Buturi, na ndipo alipokua ameishi muda wote wa uhai wake.

Ibada ya kuuaga mwili , Dar es salaam

Beautiful and peaceful sendoff kwa mama yetu Yucabeth Chaulo yaliyofanyika nyumbani kwa mmoja wa watoto wake huko Mwanangati, Yombo Vituka, Dar es salaam. Kuishi maisha ya kumtukuza Mungu ni raha na amani tele! Amemaliza mwendo, tuonane asubuhi ile njema! ?? ……. Aneyeimba ni mwimbaji mashuhuri ajulikanaye kama Angela Magoti. Angela ameolewa na mjukuu wa marehemu.

“Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.” Ufunuo 14:13

Video hizi zote ni ibada ya mazishi yake leo hii 07/01/2021 huko Buturi, Rorya.

Video hii haina uhusiano na msiba huu! Japo wimbo wao huo ndio uliokuwa ukitumbuiza wafiwa.

“Bali wewe, uwe na kiasi katika mambo yote, vumilia mabaya, fanya kazi ya mhubiri wa Injili, timiliza huduma yako. Kwa maana, mimi sasa namiminwa, na wakati wa kufariki kwangu umefika. Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda; Baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake.” 2Timothy 4:5-8

Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe milele zote. Tuonane Paradiso mama yetu! ????

Video hii haina uhusiano wowote na msiba.

Leave a Reply