Strong walls shake but never collapse!

1bd9b8f0a8f850cbdeff3b758f142d92FB_IMG_1472436063790Hakuna kitu au jambo jipya hapa duniani! Vitu vingi tunavyo viona au mafundisho mengi tunayoyasikia huwa yanakua yalishawahi tokea na kusemwa huko nyuma na watu fulani! Tofauti inakuwepo kwenye namna ya usemaji au style ya maneno yanayo tumika kufikisha huo ujumbe mpaka kuonekana kama kitu kipya au kugusa hisia za watu……. Hivyo nimependa sana ujumbe hapo juu ?  hasa sehemu hiyo ya mwishoni “strong walls shake but never collapse”!! Ni ujumbe ambao nimekuwa nikiusikia katika maneno tofauti tofauti lakini haya ya leo yamenigusa zaidi!……….. anyway, duniani kuna mambo mengi na watu waaina tofauti tofauti. Wengine wabaya, wengine  wapo sawa kiasi, na wengine ni watu makatili wenye roho za Farao! Katika hao watu wapo watakao kupa furaha, wapo watakao kupa huzuni, na wapo watakao taka kukuangamiza kabisa kwasababu tu ya udhaifu wao na chuki walizo nazo juu ya nafsi zao lakini kwakuwa hawawezi jibadilisha hivyo wanaona kuumiza wengine ndio njia pekee ya wao kupata faraja! Katika hayo yote mema, mazuri, na mabaya tambua tu kuwa wewe ni ukuta imara ambao kamwe hauto anguka! Unaweza yumba kwa mtikisiko lakini hauto anguka kamwe!

Leave a Reply