Tamar Braxton amekwenda mahakamani kuomba talaka!

Nashindwa kuelewa ni kitu gani huwa kinatokea, ndani ya miezi michache watu wanakataa kabisa kuwa ndoa yao ipo sawa na hizo rumors ni maneno tu yamtaani!! Wanathubutu hata kumtaja Mungu!! Halafu hamjakaa sawa mnasikia wame file for divorce kuwa wameshindwana! Sasa najiuliza why lying!?! Kama ndoa inamatatizo si unasema tu, kuwa ndoa yetu haipo sawa lakini we are working on it, just pray for us!! Kuliko kudanganya!! Kama hapo ?kwenye video Tamar na mumewe walivyo jieleza kwenye Wendy Williams show mwezi wa tatu mwaka huu embu wasikilize

Kana kwamba hiyo haitoshi hata mwezi uliopita alipo ulizwa akasema yupo teyari kufanya chochote kile kulinda ndoa yake. Na hivyo kitu chakwanza ambacho anafanya ili kuokoa ndoa yake ni kuachana na "showbiz business" ataacha kutengeneza album za nyimbo mpya! Sasa within 30 days inakuwaje mtu huyo huyo ndio anakuwa wakwanza kudai talaka ??  I don't get it!.......

Lakini ukiangalia kwaundani utagundua huyu Tamar kuacha kuimba siyo kwasababu alikuwa anataka kuokoa ndoa yake bali ni njia ya kumuondoa mumewe kuwa Manager na producer wake. Kama mnakumbuka how Lady JayDee alivyo mfanyia Captain Garnder Habash ?? smart lady huh! .......Jamani let your husband be your husband! Mambo ya mumeo kuwa Manager wako kwakweli naona ndoa nyingi zinavunjika ni wachache mno wamefanikiwa. Labda kama huyo mumeo hachukui pesa yoyote kwenye hiyo production yako. Your husband / wife is your business partner and advicer but not someone to manage you everyday, no no! You can only meet at the board meetings or kwenye weekly business meeting. Lakini kila mtu awe na ofisi yake na wafanyakazi wake nafikiri kwa njia hii itapunguza tension fulani zisizo na ulazima!

Halafu pia kitu ambacho nimeona wanandoa wengi ambao wako kwenye the same industry ndoa zao hazidumu au zinakuwa na matatizo sana. Kwamfano, hapa Tamar ni muimbaji na reality TV star wakati mume wake ni producer mkubwa kwenye music na TV show hivyo wote wapo kwenye spotlight na mzunguko wa watu hao hao kila wakati! Lazima wanandoa wawe makini sana mnapokuwa kwenye maswala ya business ili ndoa yenu iwe na amani.  Sasa Tamar na Vince walipo owana hawakupeana "prenuptial agreements" kwani walikubaliana kuwa divorce is NOT an option! Sasa pale divorce inapokuwa ni the only option sijui itakuwaje kwani Tamar anataka full custody ya mtoto wao na pia anasema Vince asipewe spouse support. Kumbuka wakati Tamar anaolewa na Vince, Vince ndio alikuwa anatengeneza pesa nyingi lakini baadaye Tamar akawa super star na kutengeneza pesa nyingi zaidi ya Vince hivyo sasa itabidi Tamar amlipe Vince pesa za kujikimu baada ya divorce..... Vince ni yatima na kwao alizaliwa mwenyewe hivyo hana ndugu wa tumbo moja wala wazazi! So sad!

Couple nyingine ambayo imeshangaza watu ni ya huyu mwanadada wa The Real talk show ?? Jeanie Mai na mumewe Fredy! Hapa mwanamke ndiye aliyesema kuwa yeye hataki kuwa na watoto kwani haoni kama atakuwa mama mzuri kwani kulea kiumbe kingine na kumfanya awe ni kiumbe bora is a tough job ambayo yeye hawezi. Pia kwasasa yupo busy na "carrier" yake wakati mumewe anataka wazae watoto kitu ambacho hawezi fanya. Kutokana na history yake ya kutoka kwenye familia duni wazazi wake waliangaika sana wakaja Marekani kutafuta maisha bora haswa kwa watoto wao. Hivyo kuwa na watoto kuta slow down dream zake ambazo yeye na wazazi wake wameteseka sana kuzipata. Nabado kuna watu masikini kwenye familia yake ambao anaona kuwa anawajibu wa kuwasaidia hivyo kuleta watoto duniani itakuwa ni mzigo mwingine wa watu wanao mtegemea! Hayo ni maisha ya Marekani kule kwetu Africa masikini ndio wanazaa zaidi ya matajiri wanajua mjomba/ baba mdogo au shangazi atawalea tu bila shida ??

Hivi, mimi nashindwa kuelewa hivi dunia hii kunawatu wanaowana bila kujadili kama wanataka watoto au hapana!! Hivi si vitu vinajadiliwa kabla hata ya kuchumbiana au mie ndio sijui ?? nielewesheni ?? mie I would love to know what am I signing up for, sorry naogopa sana kujifunga kitanzi mwenyewe! Naogopa surprises .........Kumbuka Tamar Braxton alikuwa kwenye show hii kabla ya ufukuzwa mwaka jana!

 

Leave a Reply