Usisahau malipo ni hapahapa- Chris Mauki

USISAHAU MALIPO NI HAPAHAPA!!FB_IMG_1473124420369Hivi unanini wewe? umeolewa kama wanawake wengine, umemkuta mumeo anawatoto unaanza kuwa adui kwao na kuwatenganisha na baba yao. Au umeolewa baada ya mumeo kuachana na mke wa awali sasa umeanza kumwambia mumeo kila mabaya ya hao watoto wake na mazuri ya hao wakwako. Kiu yako ni kumweka mbali na wanae na kumfanya awapende wakwako. Kibaya zaidi unawashawishi wanao wawachukie hao watoto wa mumeo, eti unawaambia kuwa wao wanashea baba ila mama ni tofauti na kwamba wajiepushe nao sio watu wazuri. Hivi nia yako hasa ninini? Haujui kwamba kila ulipandalo utalivuna? Hujui kwamba “what goes around comes around?”. Usijefikiria ndio umefika, hujui hata kwanini mwenzako alitoka, nawewe unaweza kutoka vilevile – Chris Mauki

Leave a Reply