Uzalendo huanzia nyumbani kwako!

"Picha hii ilipigwa siku ambayo nilitangaza kuwa sitagombea tena Ubunge, baada ya kuwatumikia kwa miaka 10. Sita sahau hisia zetu siku hiyo, jinsi mioyo yetu ilivyo vunjika kwa kujua kuwa mazoea yetu yatabadilika. Nina uhakika upendo wetu umebaki daima. Ndugu zangu Singida mjini ninawakumbuka sana! ❤ MO" // This picture was taken the day I announced to my constituents that I won’t be running for parliament, after serving them for 10 years. I won’t forget our emotions that day, a deep sense of heartbreak knowing that our interactions will change but the love will forever remain. My fellow Singida Urban brothers and sister, I miss you dearly! ❤️ MO"

Biblia inasema kuwa mtu asiyependa wakwao ni mbaya kuliko mtu asiye amini! Yani ni bora  mpagani anaonekana mtakatifu mbele za Mungu kuliko yule anaye sema anamuamini Mungu wakati anachukia na kutojali wakwao! Kuna watu wengi sana tena wengine wapo mbele ya macho yetu kila siku baadhi yetu wanawachukulia kama "role model" wao bila kutafakari kwa kina kuhusu hao "role model" zao! Je,  umewahi kuwachunguza kama kweli wanapenda wakwao? Au ni watu wa 'mikakati' yani they have an hidden agenda ya kutaka kupata pesa kutoka kwa wazungu na sponsors wa mambo yao! Kama ni kusaidia je  umeshaona wakisaidia wakao? Au ndio wale watu ambao ndugu zao wote ni wa "mujini wenye pesa" ukiishi uswahili kwetu kule Keko wewe siyo ndugu yao hawakujui!! Uzalendo unaanzia nyumbani kwako kwani hata hao ndugu zako ni Watanzania hivyo ukiwasaidia unasaidia taifa la Tanzania. .............Binafsi naheshimu nakupanda  watu wenye tabia ya kutoa jasho lao na kusaidia watu bila kuomba au kubugudhi wengine. Mfano ni Mh. MO Dewji, ShyRose Bhanji, Dr. Ntuyabaliwe  Foundation, Rita Paulsen, Flaviana Matata Foundation, Kidoti na wengine. Sipendi mtu anayetaka kusaidia wengine kwa kulazimisha wengine wamchangie kwani kusaidia mtu ni ibada, hivyo ni siri ya mtu na Mungu wake. Usinielewe vibaya kuna kuchangia kwingine naunga mkono kabisa kama mambo ya cancer, shule, n.k (for special cause). Ninacho ongelea hapa ni kusaidia watu binafsi......... Anyway, napenda vile Mh. MO anavyo wajali watu wa kwao huko Singida mjini. Mfano mzuri wa kuwa uzalendo, unaanzia ndani ya nyumba yako!

Leave a Reply