“We should all be feminists”!

FB_IMG_1473093617363FB_IMG_1472436063790Ni aibu sana kuona kuwa tupo 21st century na bado haya mambo yanatendeka! Kwamba wanawake hawatakiwi kuwa na ndoto za kufanya vitu vikubwa kisa hato olewa??!! Really! Asipo olewa anakuwa si mwanamke kamili!! Akiolewa hajazaa basi ndoa yake batili!! Akiolewa , kazaa watoto wa kike tupu bado anaonekana hajazaa!! ……….Akifanya mambo makubwa eti huyo uhuni ndo umemsaidia!! Kwakweli sauti ya mwanamke wa Kiafrica bado haina nguvu kabisa siyo tu katika jamii bali hata ndani ya familia nyingi!! Na hili swala halitaisha kama bado familia hazijatambua na kuona thamani ya mtoto wakike kuwa ni sawa na ya mtoto wa kiume! Haya matatizo yote yanayo husiana na mambo ya jamii huwanzia ndani ya nyumba na tiba yake huanzia nyumbani! Pia vile vile ni ngumu sana kukabiliana na hizi changamoto kama bado tunawachagua viongozi wakiume kusimamia mambo ya wanawake!!………Tafakari, fanya mabadiliko! 

Leave a Reply