Zamaradi Mketema: Simama kwenye sehemu ambayo hata mtu aamue kujiongeza kwa namna gani asiweze kusimama kwenye sehemu yako

Regrann from @zamaradimketema - Wanaofanikiwa kuonekana haraka mara nyingi ni wale walio kwenye makundi ya peke yao, na zaidi kuonekana kwao kunadumu. Hakikisha unakuwa wa tofauti kiasi akose wa kulinganishwa na wewe, usiende na crowd. Usifanye kama wanavyofanya wote, usiige njia za wengine, wala usilazimishe identity zilizokuwa zimeshafanikishwa na wengine (zisizokuwa zako). Simama kwenye sehemu ambayo hata mtu aamue kujiongeza kwa namna gani asiweze kusimama kwenye sehemu yako. Iwe inaangaliwa kwa jicho lolote mtu atakaloamua kuiangalia lakini ibaki kuwa yako, ikizungumziwa hiyo sehemu wakuwaze wewe kwanza, na si kuwa NYONGEZA baada ya wenye kuaminiwa nayo kutajwa kwanza, na hakikisha unaifanya iwe sehemu ambayo SIO kila mmoja anaweza kuifika kwa KIWANGO CHAKO pale anapoamua, kusaidiwa au kuoneshwa. Na kwa bahati nzuri kila binaadamu anayo sehemu hii ila kwakuwa wengi wamejawa na hamu za kufanya kama wengine wanajikuta wanachelewa kwenye njia zao, achana na njia zitakazokuchelewesha na kukufanya uonekane mdandiaji, tafuta yako kisha uivae inavyostahili.

 

Leave a Reply