Hili halikubaliki! Mh. Paul Makonda tafadhali fuatilia hili!

 Nimesha sema mara nyingi na siku zote nitasema kuwa mimi si mwanasiasa nawala sitegemei kuingia kwenye siasa, na wala hata siku moja sitamtetea mwanasiasa yoyote yule! Mambo ya siasa nawaachia mwanasiasa wenyewe wateteane! Lakini naomba ieleweke kuna mambo ambayo yataniwia vigumu kunyamaza kama hill la kwenye video! Nahapa nitaongea kama Mtanzania, na kama mama! ……….Kwakweli hili swala limenihuzunisha sana! Hii hali siyo yakukubalika haswa katika karne hii ya 21! Nikiwa kama Mtanzania niliyezaliwa katika mazingira duni na wengi wa ndugu zangu bado wanaishi kwenye mazingira duni  hivyo, hawa watoto licha ya kwamba ni Watanzania yawezekana pia wakawa ni watoto wa ndugu zangu!! Hivyo siwezi kunyamaza kwa hili! Lazima jambo kama hill linalo hatarisha maisha ya watoto zetu likemewe na lipigwe marufuku mara moja!! Ni juzi tu tumepoteza watoto 32 wa LuckyVincent sec school (somahapa) halafu bado tu mambo kama haya ambayo yanahatarisha uhai wa watoto wetu hayajakemewa na kuweka sheria kali!?! Ni lini tutajifunza kuzuia majanga na siyo kutibu!! Watoto wanatakiwa kwenda shule kusoma siyo kutafuta na kubeba maji visimani!! Huu ni unyanyasaji wa watoto na kuwakatisha tamaa ya kusoma!! My brother Paul Makonda nimesikia hii ni Kinyerezi ambapo ipo ndani ya Mkoa wako, tafadhali naomba ufatilie hili swala!

#Mungu ibariki Tanzania. Mungu ibariki Africa!

Leave a Reply