“HIVI KWELI HILI NDILO OMBI LA WATU WENYE ULEMAVU KWA MH. JPM?” ~~~~ Peter Sarungi

HIVI KWELI HILI NDILO OMBI LA WATU WENYE ULEMAVU KWA MH. JPM?fb_img_1479740222055Jana ilikuwa siku muhimu sana kwa makundi mbalimbali ya kijamii kama wakulima, wafanyakzi, watoto, wanasiasa, wavuvi, wazee, vijana, wanawake, wafanyabiashara na makundi mengine yanayo endana na hayo. Mimi nilikuwa mmoja kati ya wengi waliokuwa na hamu ya kusikia neno kutoka kwa JPM linalohusu jamii yangu ya watu wenye ulemavu Tanzania.

Kwa bahati nzuri katika fani ya uandishi wa habari, tunaye mwandishi wa habari bora kabisa aliweza kupata tuzo mbalimbali za ndani na nje ya nchi kutokana na makala na uandishi uliohusu maisha ya kila siku ya watu wenye ulemavu. Mwandishi huyo nguli anaitwa #Tuma_Dandi kutoka Chuo kikuu cha Dar es Salaam – Jounalism school. Hivyo moyo wangu ulikuwa umejiandaa kupata maswali/swali litakalo gusa changamoto kubwa kabisa za mtu mwenye ulemavu Tanzania. Tuna mshukuru sana Ndugu yetu #Tuma kwa utayari wake na kwa nia yake ya kusema maswala ya watu wenye ulemavu wakati wowote na kwa fursa yoyote.

Ninavyo amini mimi, kupata nafasi huru ya kumuuliza mkuu wa nchi swali ni nadra sana na ikitokea ukapata nafasi hiyo basi ni vizuri ukaitendea haki kwa kuuliza swali muhimu kwa jamii yako. Hivyo niliamini kuwa Mwandishi wetu Nguli angeuliza swali ambalo ni specific katika sector flan ambayo imekuwa na kero lakini kwa mshangao mkubwa, mwandishi wetu hakuuliza swali bali alitoa ombi juu ya utekelezwaji wa sera na sheria namba 10 ya watu wenye ulemavu. Maombi hayo yasiyokuwa na kero yalikuwa kama ushauri kwa Mkuu wa nchi ingawa naamini kuwa Mkuu wa nchi anaijua sheria hii na ndio maana akaweka wizara maalumu ya kishugulikia maswala ya watu wenye ulemavu. Kwa mtazamo wangu ule mkutano ulikuwa rasmi kwaajili ya wahariri kuhoji utekelezaji wa JPM kwa kipindi cha mwaka tangu achaguliwe kuwa mkuu wa nchi.

Mkuu wa nchi aliyapokea maombi hayo na kuelezea vizuri sana ni jinsi gani anavyo jali watu wenye ulemavu na hata kutaja viongozi wenye ulemavu alio wateua katika nydhfa mbalimbali ikiwemo nwibu waziri. Kwa majibu haya mazuri ya JPM ni dhairi kuwa kazi iliyobaki ni ya watendaji wake wakiongozwa na viongozi wenye ulemavu walio teuliwa. Wao ndio wana jukumu kubwa la kusukuma maendeleo ya kundi hii na hapo ndipo mwandishi wetu angeweza kupata maswali mengi ya utendaji yanayo gusa kero za watu wenye ulemavu kama vile ajira, elimu, uchumi, ujasiriamali, ushirikishwaji, afya na huduma zingine ambazo zimeendelea kuwa ngumu kwa kundi hili huku wizara yake ikiendelea kukaa kimya.

Kimsingi Mkuu alitaka kupima uwajibikaji wa wasaidizi na watendaji wake kwa mwaka mmoja kupitia maswali ambayo angeulizwa na yeye kutoa majibu.

Peter Sarungi (Next Speaker-Baba Pilato)
Peter Sarungi (Next Speaker-Baba Pilato)

#Mytake
Mh. JPM, jamii ya kundi hili hatukuwa na ombi hilo pekee lililoletwa na mwandishi wetu bali tulikuwa tunaka kuhoji kama ifuatavyo.

Tulipiga kelele sana iliyopelekea kuanzishwa kwa sheria namba 10 ya watu wenye ulemavu mwaka 2010 tukiamini kuwa sheria hiyo ndiyo mkombozi wetu, Ni miaka sita tangu sheria hiyo kuanzishwa bila utekelezaji, Je, serikali yako imefanya jitiada gani kwa kipindi cha mwaka mmoja kuhakikisha sheria hii inatekelezeka ki uhalisia? na je serikali yako ina mkakati gani ya mbele kuhakikisha sheria hii inendelea kutekelezwa?

Kwa swali hili naamini tungepata majibu ya JPM yenye kulenga utekelezaji uliofanyika na hata tungejua ni kipi kinenda kufanyika juu ya sheria hii, pamoja na hayo, swali lingewafumbua macho watendaji na wasimamizi wa wizara husika kuhakikisha wanaendelea kutilia mkazo utekelezaji wa sheria hii.

Asanteni sana
0713037798

Leave a Reply